WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako leo amezindua mradi wenye thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni 200 unaojulikana kama Elimu na Ujuzi kwa ajili ya kazi na
uzalishaji, (ESPJ) kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo
mkoani Arusha.
Akizungumza katika uzinduzi huo Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza rasilimaliwatu yenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,Utalii,Ujenzi ,nishati na madini watapatikana kwa wingi.
Alisema
kuwa Miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vine vya umahiri katika masuala
ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu,ikiwemo viwili vinavyomilikiwa na Chuo
Kikuu cha Technolojia cha Nelson Mandela cha Arusha pamoja na vituo vingine viwili
vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine University of Agriculture cha
Morogoro.
![]() |
Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa
Joyce Ndalichako akiandamana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo
(kushoto) na viongozi wengine, akiwasili katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia
cha Nelson Mandela cha Arusha ambapo amezindua mradi wa Vituo vya Umahiri
utafiti wa kilimo na Magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa
kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia
Bella Birds amesema, uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana
utasaidia taifa kufikia malengo yaliyokusudiwa na baadae kufikia uchumi wa
viwanda.
Mkurugenzi
huyo amesema pia kwamba, inakadiriwa kuwa Vijana takribani zaidi ya milioni 1
huitimu katika vyuo na kuingia katika soko la Ajira kila mwaka hivyo anatarajia
kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo
zitashirikiana vyema na serikali .
Nae
Makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Karoli Njau
alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo
yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye ameeleza pia kwamba TPSF ina upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini ambapo huchangia kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Bwana
Simbeye aliongeza zaidi kwa kubainisha kwamba, waajiri hulazimika kuajiri watu wenye
ujuzi kutoka nje ya nchi jambo linalogharimu fedha nyingi, hivyo mradi huo
utasaidia vijana zaidi ya 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la
ajira.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment