AFYA ZA WAKAZI MJI WA DODOMA HATARINI. - Mazengo360

Breaking

Tuesday, 28 November 2017

AFYA ZA WAKAZI MJI WA DODOMA HATARINI.

AFYA za wakazi  wa Manispaa ya Dodoma zipo hatarini kushambuliwa na milipuko ya magonjwa baada ya mamlaka mbili kutupiana mpira nani mwenye dhamana ya utunzaji afya ya mazingira.

Sura ya Mji wa Dodoma. 

Manispaa ya Dodoma ndio yenye dhamana ya kusimamia na kudhibiti vyanzo vya milipuko ya magonjwa na TARURA ambayo ni taasisi mpya inayosimamia na kutunza barabara za mitaani na vijijini kwa sasa inaendeleo na ujenzi katika mitaa ya manispaa ya Dodoma.

Kulingana na hali halisi ilivyo kwa sasa katika mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Uhuru Manispaa ya Dodoma hali ya afya ya mazingira za wakazi hao ni mbaya na hatarishi hususani kwa sasa mvua za masika zinapoanza kunyesha kuanzia jana mjini humo.


Baadhi ya Nyumba na Biashara zilizoathiriwa na maji taka mtaa wa Mji Mpya Dodoma.

TARURA Mkoa wa Dodoma katika ukarabati wa barabara za mtaa huo,ni takribani mwezi mzima sasa mkandarasi amefukua miundombinu ya maji safi na taka katika barabara za mtaa huo na kuziacha bila kuirekebisha, hali ambayo maji taka yenye kinyesi yamekua yakizagaa ovyo mitaani na kuzua kero hata wafanyibiashara wengine kushindwa kufungua biashara zao.

Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Mr Godwin Kunambi hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita muda mrefu kisha kupokelewa na msaidiazi wake na kusema yupo kwenye kikao.

Baadae alipatikana Afisa Mahusiano wa Manispaa hiyo Mr Ramadhani Juma, lakini baada ya kuombwa kutoa ufafanuzi juu ya hali katika mtaa wa Mji Mpya alisema Ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma ndio yenye majibu hayo.

“Mwenye dhamana na majibu ya hali hiyo sio Manisapaa bali ni TARURA Mkoa wa Dodoma, waulize watakupata majibu” alisema Afisa Uhusiano huyo.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mratibu wa TARURA wa Mkoa wa Dodoma Injiania Mohamed Mkwata zilizaa matunda baada ya kumpata kwa simu akiwa Bagamoyo kwenye mkutano.


Baadhi ya Barabara za Mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Uhuru Manispaa ya Dodoma baada ya kushindiliwa kifusi   kwa awamu na Mkandarasi ambaye yupo chini ya usimamizi wa TARURA Mkoa wa Dodoma, lakini hakuna udhibiti wa maji taka yanayosambaa ovyo yenye vinyesi katika mtaa huobaada ya miundombinu ya mabomba kuharibiwa wakati wa ukarabati huo.

Injiania Mkwata amesema, kwa sasa yupo Bagamoyo lakini anachojua ni kwamba vifusi vilivyomwagwa katika mtaa wa Mji Mpya vinaendelea kusambazwa na kushindiliwa kwa awamu,lakini akashindwa kutoa jibu la maji taka na kusema aulizwe Injinia wa Manispaa ya Dodoma.

Muulizeni Injiania wa Manispaa ya Dodoma ndiye niliyemwachia jukumu la kusimamia mradi huo anayo maji” alimalizia nakukata simu Injinia Mkwata.
Inavyoonekana kuna hali ya kutupiana mpira kati ya Manispaa ya Dodoma na TARURA ingali afya za wakazi zipo mashakani na msimu wa mvua tayari umeshawadia.

Pia mtaa wa Mji Mpya upo mkabala na Uwanja wa mpira wa Jamhuri Mjini Dodoma ambapo pia vikosi vya majeshi yetu  Ulinzi yakiwamo Polisi, Magereza na JKT yameanza kuweka kambi katika uwanja wa jirani wa shule ya Sekondari ya Central ya mjini Dodoma ili kujifua kwa sherehe za Uhuru December 09, ambapo kitaifa zinafanyika hapa Dodoma na Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri Dkt John Pombe Magufuli.

Idadi ya watu wanaofanya shughuli zao na kupita katika mtaa huo ni kubwa ambapo pia wanaoshuhudia mazoezi hayo na wengi hivyo kuziweka rehani afya za wakazi hao.


MWISHO. 

No comments:

Post a Comment