SEREKALI inajadiliana na
wataalam wa mradi wa uzalishaji Umeme kwa njia ya sumaku kutoka Ujermani ili
kuongeza upatinaji wa Nishati hiyo zaidi hapa nchini.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akimkaribisha ofisini kwake mtaalum wa Umeme Sumaku kutoka Ujermani jioni hii leo mjini Dodoma. |
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amekutano na wawekezaji hao leo jioni November
13, 2017 hapa mjini Dodoma katika ofisi za Wizara hiyo ya Nishati.
Baada
ya kuzungumza na Waziri, wawekezaji hao kutoka Kampuni ya Tangen Investment
Limited ya Ujerumani, wamefanya majadiliano na wataalam wa nishati kutoka
wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma
za Nishati na Maji (EWURA).
Wawekezaji
hao wametakiwa kuwasilisha Andiko la Awali (concept note) la Mradi wao ili
lipitiwe na kujadiliwa na wataalam husika, kabla ya kuendelea na hatua nyingine
stahiki za uwekezaji nchini.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment