SEREKALI kuanza kumchunguza
aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati wa serekali ya awamu ya nne Mhe Lazaro
Nyalandu endapo hakua muadilifu wakati wa madaraka yake.
Mhe Lazaro Nyalandu. |
Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliambia Bunge leo mjini Dodoma na amelitaka jeshi la Polisi na TAKUKURU kumchunguza endapo Mhe Nyalandu alitumia vibaya madaraka yake wakati wa uongozi wake au lah.
Kigwangalla
ametoa kauli hiyo alipokuwa akichangia hoja ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2017/2018
na kusema kwamba, “wakati wa uongozi wake Lazaro Nyalandu
aliikosesha serikali mapato ya bilioni 32 kwa kutosaini sheria ya tozo kwa hoteli
za kitalii”.
Mbali
na tuhuma hizo, Waziri Kigwangalla pia amesema Lazaro Nyalandu akiwa
Waziri alitumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni kwenye kampeni zake
mwaka 2015 wakati kampuni hiyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.
Mhe
Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM)
alijiuzulu nafasi zake zote ikiwamo uanachama wa Chama cha Mapinduzi hivi
karibuni na kwa sasa anasadikwa kujiunga na chama cha upinzani cha CHADEMA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment