Judith Daines Wambura Mbibo ni mwanamuziki wa Bongo Flava-Afro Pop kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Lady Jay Dee.
Anataraji kufanya ziara ya kuwatumbuiza Mashabiki wake Mkoani Kagera kuanzia July 21 hadi 23, 2017 ambapo ataanzia wilayani Muleba Ijumaa July 21, 2017 katika ukumbi waNULPHIN HOTEL kwa Kiingilio cha Tsh.5,000/= tu.
Wilayani Ngara ni Jumamosi ya July 22, 2017 katika Ukumbi wa MOORLAND PREMIER HOTEL’S kwa kiingilioa cha VIP Tsh.8,000/= na Kawaida Tsh.5,000/=
Wakati siku ya Jumapili July 23, 2017 atamalizia ziara yake Wilayani Karagwe katika Ukumbi wa KDRDP kwa kiingilio cha Tsh.5,000/= tu.
No comments:
Post a Comment