VITUKO VYA MECHI ZA KLABU BINGWA ULAYA. - Mazengo360

Breaking

Friday, 29 September 2017

VITUKO VYA MECHI ZA KLABU BINGWA ULAYA.

JUMA hili huko ulaya kwenye mashindano ya UEFA hatua za makundi, kumeibua vituko baadhi ambapo shabiki wa mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi alipagawa na kuvamia uwanjani na kubusu guu lake la kushoto.

Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Leonel Messi ambapo shabiki wake alipagawa na kuingia uwanjani na kubusu guu lake wa kushoto wakati wa mechi ya UEFA baina ya Barcelona na Sporting CP hivi majuzi. 

Pia klabu ya PSG ya Ufaransa imesababisha kibarua cha kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti kumponyoka baada ya bodi ya klabu hiyo kumtimua kazi baada ya kipigo cha bao 3-0 hapo jana.

Ni wakati mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya unaendelea, ambao uliwakutanisha Barcelona na Sporting CP aliingia shabiki uwanjani na kumkumbatia Messi kisha kumbusu mguu wa kushoto, kabla ya Askari wa uwanjani (STEWARDS) kumtoa nje shabiki huyo.

Cha ajabu wakati huohuo mashabiki wa Sporting CP walikuwa wakiimba Ronaldo Ronaldo uwanja mzima.

Sporting CP, ndio ilikuwa klabu ya kwanza kuchezea staa mpinzani mkubwa wa Messi ambaye ni Christiano Ronaldo.

Baade Barcelona ilishinda mchezo huo kwagoli 1-0.


Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti, ametimuliwa kazi.

Wakati huo huo kufuatia kichapo cha goli 3-0 dhidi ya PSG , bodi ya klabu hiyo iliamua kumfuta kazi kocha wake Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italy aliyerithi mikoba ya kocha Pepe Guardiola tangu msimu uliopita.

Ancelotti mwenye umri wa miaka 58, aliisaidia Bayern Munich kushinda taji la Bundesliga, lakini hawakuweza kufika katika raundi ya mtoano ya kombe la vilabu bingwa pamoja na nusu fainali ya kombe la Ujerumani.

Kwa sasa atakayeongoza klabu hiyo ni Naibu meneja wa klabu hiyo Willy Sagnol, ila zipo tetesi kwamba bodi hiyo ina mnyatia kocha wa Liverpool ya Uingereza, Jurgen Klopp ambaye pia ni raia wa Ujerman. 

Bayern Munich wako katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi , wakiwa na alama tatu nyuma ya Borussia Dortmund, ambapo wameshinda mara nne.

MWISHO.


No comments:

Post a Comment