IJUE NGUVU YA MSAMAHA. - Mazengo360

Breaking

Thursday, 28 September 2017

IJUE NGUVU YA MSAMAHA.

KATIKA tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawafikii au kupata maendeleo yao binafsi wanayo kusudia kwa sababu hawatambui nguvu ya msamaha ilivyo kubwa katika safari ya Mafanikio yao. Hali kadhalika tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zao.

Mtu mwenye msongo wa mawazo (stress) kwa kutosamehe wengine.

Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna aliye sabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inaonekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya leo, kesho mpaka kesho kutwa usiweze kuyasahau.

Maneno au vitendo hivyo hukusababishia kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, na hata kuleta magonjwa na mawazo mengi (stress).

Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutosamehe yanavyoweza kumuathiri mtu;

Usipo  samehe kunakufanya  kwa kiwango kikubwa kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kuna sababisha kuzama katika dimbwi kubwa la mawazo.

Hata hivyo mawazo hayo hayo yanakusababishia kujikita katika tabia zisizo za kimaadili kwa mfano ulevi, wizi na mengineyo mengi. Na pindi mtu atendapo mambo hayo ambayo chanzo chake huwa ni mawazo, madhara yake huwa ni makubwa kama nilivyoweza kuanishwa hapo juu.

Basi bila kupata kigugumizi cha kusoma makala hii hebu tujaribu kusoma kwa umakini na uingie zaidi katika kilindi cha nafsi yako halafu jiulize umebeba vitu gani juu ya watu wengine?

Kisha jaribu kutafakari kwa umakini tena mambo hayo yamekuathiri kwa kiwango gani?
Baada ya kupata majibu sahihi juu ya tafakari hiyo, jaribu kuzama tena katika mishipa ya ubongo wako kisha tafakari bila ya kujionea huruma kwa hisia kwamba utachukua hatua gani juu ya swala hilo.

Majibu sahihi ambayo utakuwa umeyatafakari ndiyo ambayo yatakufanya uweze kuona mwangaza kwenye giza na kupata mang’amuzi ya kujua ni wapi ambapo unatakiwa kuelekea ili uwe na faraja.

TUZIANGALIE FAIDA ZA KUSAMEHE.

1. Huongeza furaha ya moyo(piece of mind).

Kusamehe aliye kukosea humfanya kuwa huru kwa kila jambo ambalo unalifanya.

Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba watu wengi tumebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zetu, hata hivyo kutoka na mizigo hiyo mizito tunashindwa kupiga hatua za kimafanikio.

Hivyo inatubidi  kuwaza hatua za mafanikio hivyo hatuna budi kujifunzanjia za kuwasamehe watu wengine waliowahi kutukosea .

Mafundisho kutoka katika vitabu vya dini vinatukumbusha ya kwamba Mungu tabia yake ni kusamehe, hivyo nasi hatuna budi kusamehe wengine.

 Vitabu hivyo hivyo vya dini vinatueleza ya kwamba tusamehe kwa saba mara sabini, yaani tutoe msamaha kwa wengine bila ukomo na endapo utapata  ujasiri wa kusamehe unafungua milango ya mafanikio yako.

2. Kusamehe ni njia ya mafanikio.

Endapo leo utaamua kusamehe ni ishara ya kujitoa katika sakata la kuwa katika wimbi la mawazo.

Pia kutakufanya uwe na mawazo chanya na mara kadhaa watu ambao hawana ule moyo wa msamaha kwa namna moja ama nyingine huwa katika msongo mkubwa wa mawazo na hukosa kabisa amani.

Hata hivyo, kama kweli unataka maisha yawe sawa ni muda wako sahihi wa kuvijua vile vyote vilivyomo katika nafsi yako vinavyokufanya ukose amani kinyume cha hapo utakuwa unazidi kupotea na haijalishi ulikwazika kwa kiasi gani.

Pia ukumbuke wabaya wetu ni binadamu kama sisi na pia watu hao hao ndio majirani zetu na wana mchango mkubwa katika safari yetu ya mafanikio.

3. Kusamehe huimarisha afya.

Afya njema ni njia ya kupata mafanikio na moja ya kanuni ya kutaka kupata mafanikio ni kwamba unahitaji kuwa na afya njema ili uweze kuimarika na kuwa na mtizamo ulio sawa.

Hebu tutafakari kidogo hivi leo ukipata ugonjwa wowote na kukufanya usiweze kuendelea na kazi yako, jiulize huwa unaathirika kwa kiasi gani katika majukumu au mipango yako?

Kama umepata majibu nafikiri utakuwa umeona umuhimu wa kuwa na afya njema.

Tuangalie mfano mmoja, watu wengi hawana hamasa za kiutendaji wa mambo mbalimbali kwani ni dhahiri ya kwamba miili yao tayari imeathiriwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na mawazo mfano shinikizo la damu au sukari ambapo husasabishwa na watu wanaokuzunguka.

Magonjwa haya yataondoka tuu enadapo utamua kuwasamehe watu ambao waliwahi kukosea na kuwa katika misingi ya kuimarika kiafya kiujumla, ambapo  kufanya hivyo kutakufanya uweze kuongeza uwezo wako wa kufikiri na hata kukufanya kupiga hatua mbele za kimafanikio.

Hivyo tambua na elewakila mmoja  anahitaji nguvu ya msamaha kwa wengine kwani hatuwezi kuishibilamakwazo na wengine, hivyo itakufanya uweze kupata mafanikio ya kweli katika shughuli zetu za kila siku.

Pia tuelewe katika maisha ya mwanadamu, Mungu huchukua sehemu kubwa sana ya uhai na mafanikio yetu pia, hivyo nimuhimu sana kujua nguvu ya msamaha.


MWISHO.

No comments:

Post a Comment