MWANADAMU
aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye
huchanua kama vile ua, kisha hukatwa, wala hakai kamwe.(Ayubu 14:1-2)
Bi Rose Athumani wakati wa Uhai wake. |
Maneno haya kutoka kwenye
maandiko matakatifu kitabu cha Bibilia, si kwamba yaliandikwa kwa madhumuni
mengine bali ni kwa ajili binadamu kukumbusha mahusiano yake na muumba wake
Mwenye Mungu.
Tuna huzunika na kuomboleza
kifo cha mpendwa dada yetu na kwa wengine ni mama, kilichotokea mapema asubuhi
ya jana November 09 kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa
muda mfupi.
Ni kipindi kigumu kwa
waliobaki hususani familia, jamaa, marafiki na pia wafanyakazi wenzake alikokuwa
akifanyia kazi. Ni wazi msiba huu umewagusa wengi mno kwani kulingana na kazi
yake kama mwandishi wa habari ambapo wengi walimfahamu.
“Ee Mwenyezi-mungu, Bwana
wetu, kweli jina lako latukukaduniani kote! (Zaburi 8:1)”
Tunamshukuru Mwenyezi-mungu
kwa zawadi ya uhai uliomjalia mpendwa wetu huyu aliyetuacha na kurejea kwa
muumba wake Bi Rose Athumani.
Nao waandishi wa habari wa
magazeti ya Serekali yaani TSN ambao ni wenye
kuchapisha magazeti ya Dailynews, Habarileo na Sport Leo wamesema mwenzao Bi
Rose Athumani ameacha pengo kubwa kwao.
Kaimu Mhariri wa Habari wa
gazeti la Dailynews Leornad Mwakalebela ambaye marehemu Bi Rose Athumani alikua
akifanya kazi chini ya usimamizi wake amesema,
“gazeti hilo limepoteza mmoja wa
waandishi waliokua wakijituma, mwenye nidhamu na mbunifu”.
Aliongeza pia kwamba, “alikuwa
miongoni mwa waandishi wa habari wenye uwezo na waaminifu niliowahi kufanya nao
kazi” alisema Mwakalebela.
Marehemu Bi Rose Athumani
alizaliwa Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka 1976.
Alipata elimu ya msingi na
sekondari nchini Kenya kuanzia mwaka 1988 hadi 1991 na baadae kusomea uhandishi
wa Habari kiwango cha taaluma ya digrii ya kwanza jijini Dar na baadae nchini
Marekani hadi 2002.
Alifanya kazi kama
mwandishi wa Habari kwa iliyokuwa Radio Tanzania (RTD) na baadae kamapuni ya
magazeti ya Mwananchi Communication Ltd (MCL) kabla ya kujiunga na TSN kama
mwandishi wa Habari wa Dailynews kuanzia mwaka 2010.
Alikuwa ana tabia ya
kipekee ya kupendwa na watu, mpole na mwenye haiba ya mwanamke ambao kwa asili
wameumbwa na huruma na upendo kwa wengine.
Maombolezo ya msiba huu
yapo kwa mjomba wake Paul Mushi huko Mbezi Mpigi Magohe na anatarajiwa kuagwa
rasmi siku ya Jumapili na kusafirishwa kwenda Moshi kwa maziko siku ya Jumatatu
ijayo.
“RAHA
YA MILELE UMPEE EE BWANA; NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI”
No comments:
Post a Comment