KOCHA
wa
zamani wa klabu ya Everton na Manchester United David Moyes, 54, raia wa
Scotish ametajwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya West Ham United ya Uingereza.
David Moyes, Kocha mpya West Ham United. |
Moyes ambaye alikuwa hana
kibarua tangu mwezi May mwaka huu baada ya kujiuzulu ukufunzi klabu ya Sunderland,
anachukua nafasi ya Mkufunzi Slaven Ballic ambaye ameifundisha klabu hiyo kwa
muda sasa.
Kulingana na taarifa
iliyotolewa muda mfupi uliopita hivi leo na mmoja wa viongozi waandamizi wa
klabu hiyo David Sullivan imesema, uongozi ulikuwa ukimuhitaji Mkufunzi mwenye
vigezo vya Moyes ili kuikwamua klabu hiyo ilipo sasa.
Klabu ya West Ham United
ipo katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi ya Premier ya Uingereza na ina
pointi 9 kwa sasa baada ya kushuka dimbani mara 11, na pia inayo kumbukumbu
nzuri ya kutandikwa magoli 4-1 na
majogoo wa Amfield, Liverpool FC nyumbani kwao weekend hii.
Sullivan amesema, “tunahitaji
mtu mzoefu, mwenye uelewa wa kutosha na ligi ya Uingereza ya Premier na ambaye
anawajuwa wachezaji vizuri hivyo tunaimani Moyes nimkufunzi sahihi atakayeweza
kuitoa West Ham United hapa ilipo” alifafanua kiongozi huyo.
Slaven Ballic, Mkufunzi aliyetupiwa virago na West Ham United. |
West Ham United ni moja ya klabu za ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikifanya vizuri kwa kiwango cha wastani muda wote wakiwa na Mkufunzi wao huyo Slaven Ballic na hata kufanikiwa kuzisumbua baadhi ya klabu katika ligi hiyo ikiwamo Liverpool, lakini mwaka huu mambo yamewaendea kombo.
Moyes amepewa mkataba wa
miezi 6 na kipimo chake cha kwanza ni hapo Novemba 19, wakati klabu yake hiyo
mpya ya West Ham itakapo pepetana na klabu ya Watford mbayo kwa sasa ipo nafasi
ya 9 na ina point 15 katika msimamo wa ligi hiyo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment