WATAALAM wa Maendeleo ya Jamii hapa nchini wametakiwa
kutoa mapendekezo serekalini yatakayosaidia kuamsha ari kwa jamii kushiriki katika mambo ya maendeleo kulingana na wakati wa sasa ili kusaidia Taifa kuingia katika uchumi wa kati kupitia viwanda.
Kauli hii imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu wakati alipokuwa akifungua
Mkutano Mkuu wa 12 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unafoanyika katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango Dodoma.
Waziri Ummy alisema “kupitia Mkutano huu wa Wataalam wa Maendeleo
ya Jamii mnatakiwa kutoa mapendekezo serekalini kuhusu mbinu zinazoendana
na kipindi cha sasa na bora zitakazosaidia kurudisha ari na hamasa ya jamii
kushiriki katika maendeleo"
Mhe. Ummy Mwalimu amesema pia wataalam wa maendeleo ya jamii ndiyo
wenye jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya kisekta hususan kilimo,
afya, elimu, na miundo mbinu na kadhalika, ili taifa liweze kwa wepesi kufikia
uchumi wa kati na wa viwanda, alifafanua zaidi.
“Wataalam wa Maendeleo ya Jamii watumie pia fursa hii kutathmini sekata ilipofikia na pia kubainisha changamoto zilizopo ili kupata majibu ya namna bora zaidi kwani mazingira ya sasa nayoni mapya yanahitaji mtizamompya kuyakabili, alisisitiza Mhe Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema Kaulimbiu ya Mkutano wa Sekta ya Maendeleo ya
Jamii kwa Mwaka 2017 ambayo ni “Amsha Ari ya Ushiriki wa
Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” ambapo inatoa tafakari ya jumla ya
Serekali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya ujenzi wa uchumi
wa Viwanda ili kufikia Uchumi wa Kati, aliongeza.
Naye Katibu Mkuu
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema agizohilo
kupitia kwa Mhe Waziri mwenye dhamana ya sekta hii ni fursa muafaka kwa
watendaji kuitumia vyema na kusaidia kuleta mabadiliko katika sekta hiyo na
kuamsha hari zaidi.
Bibi Sihaba Nkinga amefafanua kuwa malengo ya Mkutano huo
umezingatia tathmini ya mchango wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika
kuamsha ari na hamasa ya wananchi kushiriki na kuchangia maendeleo kwa
kushirikiana na viongozi wa Sekta na Idara nyingine katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewaasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na wadau kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujitoa katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo katika maeneo yao.
Lengo la Mkutano huo chini ya kauli mbiu yake “Amsha Ari ya Ushiriki
wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” inalenga kusimami maendeleo na
kutokomeza ukatili wa jinsia ambao kwa kikasi kikubwa unapunguza kasi ya Taifa
kufikia uchumi wa viwanda.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment