MAKUNDI mawili kila
moja likiwa na wastani wa wakimbizi 350 raia wa Burundi kati ya wakimbizi
13,000 ambao hadi tarehe 07 Septemba, 2017 walikuwa wamejiorodhesha kwa hiari
kurejea nyumbani yanatarajiwa kuondoka nchini wiki hii.
![]() |
Wakimbizi wa Burundi wakiwa katika
kambi ya Kigoma, Tanzania.
|
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wakimbizi, katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Deusdedit Masusu, misafara saba yenye wastani wa wakimbizi 350 inatarajiwa kuondoka nchini kurejea Burundi katika mwezi huu wa Septemba, 2017 miwili kati ya hiyo ikiondoka siku ya Jumanne tarehe 12 na Alhamisi tarehe 14 Septemba, 2017.
Bwana
Masusu aliieleza Idara ya Habari- MAELEZO ofisini kwake hivi karibuni kuwa
idadi ya wakimbizi wataorejeshwa nyumbani inatarajiwa kuongezeka kadri zoezi
hilo ambalo lilianza Alhamisi wiki iliyopita litakavyoshika kasi.
“Mpango
wetu unaonesha kuwa kwa mwezi huu wa Septemba wakimbizi waliondoka tarehe 7 na
wengine wataondoka tarehe 12, 14, 19, 21, 26 na 28 kwa watani wa wakimbizi
350”alisema lakini hata hivyo alieleza kuwa kundi la kwanza lililoondoka
lilikuwa na wakimbizi 301 tu.
Mkurugenzi
Msaidizi huyo alieleza kuwa kasi ya kujiandikisha kwa hiari kwa wakimbizi hao
raia wa Burundi inatarajiwa kuongezeka zaidi kufuatia makundi hayo kurejea
nyumbani kwa kuwa mafanikio ya zoezi hilo yatakuwa kichocheo kwa wengine kutaka
kurejea nyumbani.
“Tunatarajia
ikifika mwishoni mwa mwezi huu kasi ya kujiorodhesha itaongezeka sana kwa kuwa
watakaorejea watatoa taarifa zaidi kwa wenzao hivyo kwa wale wanaosita bila ya
shaka wengi wao hawataona sababu ya kuendelea kubaki makambini” Alisema bwana
Masusu.
Alibanisha
kuwa urahisi wa mawasiliano utawezesha wakimnizi waliorejea kuwapa wenzao
mrejesho wa hali ilivyo nchini kwao na hivyo kutoa hamasa kwa walioko makambini
nao kutaka kurejea nyumbani.
Mkurugenzi
Msaidizi huyo aliongeza kuwa kinachofanyika ni kuhakikisha zoezi hilo
linafanyika kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa ili
wakimbizi hao waweze kurejea nyumbani kwa usalama na heshima.
![]() |
Aina ya usafiri unaotolewa na Shirika la
Kimataifa la Uamiaji (IOM) katika kusaidia kuwarudisha warundi makwao.
|
“Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ndilo linalotoa usafiri wa wakimbizi na mzigo yao kutoka makambini hadi nchini Burundi na wakimbizi wanaorejea wanasaidiwa chakula kupitia Shirika la Mapngo wa Chakula (WFP) kwa miezi mitatu” Alifafanua bwana Masusu.
Zoezi
la kuwarejesha wakimbizi hao wa Burundi linafanyika kufuatia makubaliano
yaliyofikiwa tarehe 31 Agosti, 2017 jijini Dar Es Salaam kati ya Serikali za
Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi
(UNHCR).
Zoezi
la kuwarejesha wakimbizi kundi la kwanza, kwa upande wa Tanzania, lilishuhudiwa
na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (Mstaafu ) Emmanual Maganga, Kamati
ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa Kogoma pamoja Mwakilishi wa UNHCR nchini na
maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Msafara
wa Burundi uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi hiyo Theranse
Ndayiragije, Mwakilishi kutoka Ofisi ya UNHCR Burundi na washiriki wengine.
Tukio hilo lilishuhudiwa pia na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment