WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angela
Kariuki (Mb) amewasimamisha kazi maafisa waandamizi wa Halmashauri Wilaya za Kilosa na
Gairo mkoani Morogoro kwa uzembe kazini.
Maofisa hao ni Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu, Maafisa Utumishi pamoja na wale wa usimamizi taarifa za utumishi na mifumo ya mishahara (HCMIS).
Wengine ni Maafisa Elimu
Sekondari na waweka Hazina wa Halmashauri hizo.
Mhe Kariuki na Katibu Mkuu
wake Dkt Lauren Ndumbaro walifanya ziara ya kushtukiza hivi leo katika
Halmsahauri hizo baada ya kugundua kwamba maafisa hao hawakusimamia ipasavyo
zoezi la uhakiki wa watumishi hewa pamoja na vyeti feki lililo kamilika hivi
punde.
Uzembe huo uliodumu tangu mwaka 2009 na kusababisha kulipwa
mishahara ya bure Mwalimu Jasper Ibraim Luchelo wa Shule ya Sekondari Dumila
katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa tangu kipindi hicho 2009 hadi Augusti
2017 bila kuwepo kazini.
Aidha Mhe Kariuki
amevielekeza vyombo vya dola kumsaka na kumkamata Mwalimu Jasper Ibraim Luchelo
ili arejeshe fedha zote alizokuwa akilipwa toka serekalini baada ya kuomba
ruhusa ya kwenda masomoni nje ya nchi kwa miaka mitatu tangu 2009 hadi 2012
lakini hakwenda na hajaripoti kazini muda wote huo.
Halikadhalika uzembe mwingine
ni ule wa taarifa za kiutumishi na mifumo ya mishahara kwa watumishi 97 ambao majina yao
mfumo unaonyesha wanalipwa mishahara pande zote mbili za Halmashauri ya Wilaya
ya Kilosa na Gairo kwa wakati mmoja bila wenyewe kujua.
Kutokana na mapungufu hayo
Mhe Kariuki ameunda timu ya uchunguzi itakayofanya upya tathmini ya zoezi la
uhakiki wa watumishi wa Halmashauri hizo na kuwasilisha ripoti yake Ofisi ya Utumishi
mapema iwezekanavyo.
Pia Mhe Kariuki ameagiza
hata kama wahusika hao waliohusika katika uzembe huo tangu mwaka 2009 na kwa
sasa wamehamishiwa sehemu zingine serekalini au Halmashauri zingine ama kuhamia
mashirika ya Umma, waitwe kuja kujibu uzembe waliousababisha hadi serekali
kupata hasarakiasi hicho.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment