KATIKA
hali
inayoonyesha mapenzi makubwa kwa Mhe Tundu Lissu Rais wa TLS na Mbunge wa
Singida Mashariki-CHADEMA, utafiti unaonyesha wengi wamekesha kumwombea afya
njema usiku wa leo.
![]() |
Mhe Tundu Lissu, Rais wa TLS na Mbunge wa CHADEMA. |
Mhe Tundu Lissu
aliyeshambuliwa na watu wasiojukana kwa risasi alipokuwa akiingia nyumbani
kwake mjini Dodoma eneo la Area D jana mchana akitokea bungeni, taarifa ya
mapema usiku huu imeeleza afya yake inaendelea kuimarika na amehamishiwa jijini
Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi.
Taarifa aliyoitoa usiku huu
wa manane akiwa uwanja wa ndege wa mjini Dodoma wakati wa kuondoka kwenda
Nairobi Kenya, Mbunge wa Iringa Mjini-CHADEMA Mhe Peter Msigwa amesema afya ya
Mhe Tundu Lissu inaendelea kuimarika baada ya kutoka chumbacha upasuaji.
![]() |
Mhe Tundu Lissu akiingizwa kwenye ndege ya kukodi katika Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma usiku huu ambapo alipelekwa jijini Nairobo Kenya kwa matibabu zaidi. |
Amesema, “Napenda kuwajulisha kwa mara nyingine tena kwamba Lissu wetu anaendelea vizuri. Ametoka chumba cha upasuaji na hali yake inaendelea kuimarika” ilieleza taarifa hiyo fupi ya twitter ya Mhe Msigwa mapema usiku huu.
Mhe Msigwa pia amewataka
watu wote wenye mapenzi mema na Mhe Tundu Lissu wamchangie fedha zitazosaidia kugharimia
matibabu yake nje ya nchi kupitia mtando wa simu ya VODACOM kupitia M-PESA No.
0759-865 786 ya Ester Matiko, Mbunge-CHADEMA Jimbo la Tarime mjini.
Nae Kikwete Ridhiwani
ambaye ni Mbunge wa Chalinze-CCM amefanya maombi maalum ya kumwombea afya njema
Mhe Tundu Lissu na kumsii Mungu amponye haraka arudi katika majukumu yake.
![]() |
Ndege ya kukodi iliyo msafirisha Mhe Tundu Lissu kwenda jijini Nairobi Kenya usiku wa kuamkia leo ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma muda mfupi kabla ya kuondoka. |
“Mungu
Baba uliyeahidi kuipenda Tanzania na watoto wake, timiza upendo wako. Mjalie
kaka yetu Lissu afya na uzima, amina!!” Kikwete alimalizia maombi yake.
Inavyoonyesha Mhe Tundu
Lissu anapendwa na wengi ndani na nje ya Tanzania na watu wote bila kujali
umri, elimu, kipato, jinsia wala cheo ambapo mtandao huu usiku kucha umekua
ukifuatilia kwa karibu salamu zote za matashi mema kwake kupitia mitandao ya
facebook, twiiter na mingineyo, ambapo matokea yanaonyesha wazi kwamba Mhe
Tundu Lissu anapendwa zaidi na watu wote.
Salamu alizozituma Rais wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kupitia mtandao wake wa twitter, amelitaka
jeshi la polisi kuwasaka na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika kumjeruhi kwa
risasi Mhe Tundu Lissu na kuwafikisha haraka katika mikono ya sheria.
Rais Dkt Magufuli amesema zaidi
katika twitter yake fupi kwamba, anamwombea afya njema Mhe Tundu Lissu ili
arejee haraka katika afya na kazi zake, alimalizia Mhe Rais Dkt Magufuli.
Navyo vyama vya kisheria na
haki za binadamu katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki nazo
zimetuma salamu zao za kimaandishi kwa CHADEMA na kwa Mhe Tundu Lissu na
kulaani vikali tukio la kushambuliwa kwake.
Chama cha wanasheria cha
Kenya yaani “The Kenya Law Society-KLS nacho kimetuma taarifa yake ya maandishi
iliyo sainiwa na Rais wa KLS Mwanasheria Isaac N. Okero, imelaani vikali
shambulizi hilo.
Mhe Okero ameeleza katika
taarifa yake kwa Rais wa TSL kwamba “Shambulio hilo ni la kidhalimu na ni dhidi
ya Utawala wa Sheria na hivyo linapaswa kupingwa na kulaaniwa kwa nguvu zote, hivyo
kumwombea Mhe Tundu Lissu apone haraka” ilimalizia taarifa hiyo ya KLS.
Nae Naibu Mkurugenzi wa
chama cha kutetea haki za binadamu (Amnest International) Ukanda wa nchi za
Maziwa Makuu, Madam Sarah Jackson nae kimewasilsha salamu maalum za maandishi
kumtakia kheri apone haraka Mhe Tundu Lissu.
Taarifa hiyo ilitoa wito
kwa mamlaka husika yaani Serekali ya Tanzania, kufanya kila njia kuwatia
nguvuni wale wote waliohusika kumshambulia Mhe Tundu Lissu ili isionekane
kwamba shambulio hilo si la kisiasa, taarifa hiyo imemalizia.
Navyo vyama vya siasa hapa nchini
havikubaki nyuma kumwombea na kumtakia afya njema Mhe Tundu Lissu,baada ya
shambuliohilo zilizotolewa usiku wa kuamkia hivi leo.
Taarifa ya maandishi
iliyotumwa kwa CHADEMA kumtakia Mhe Tundu Lissu nafuu ya mapema na kulaani vikali
shambulio hilo, salamu za Chama cha Mapinduzi-CCM ilizosainiwa na Katibu
Mwenezi wake Mhe Humfrey Polepole zimelaani vikali kitendo hicho.
Taarifa hiyo ya CCM imeendelea
kusema kwamba, “imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kushambuliwa kwa risasi Mhe
Tundu Lissu,Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS, Polepole alifafanua.
Nacho chama cha
ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Mhe Zitto Kabwe kimetuma taarifa yake ya
maandishi kwa CHADEMA iliyosainiwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho Bwana Ado
Shaibu.
Tarifa ya ACT-Wazalendo
imewataka watanzania wote kuungana pamoja kumwombea kwa Mungu Mhe Tundu Lissu
ili apone haraka ili arejee katika majukumu yake, taarifa ya ACT-Wazalendo
ilimalizi.
Katika jambol linaloonyesha
Mhe Tundu Lissu anapendwa na wengi, taarifa takribani katika mitandao yote ya
kijamii usiku huu zilikuwa zikizungumzia taarifa ya kushambuliwa kwa risasi Mhe
Tundu Lissu.
Wengi wa wachangiaji katika
mitandao bila kujali makundi yao wala itikadi zao wamekuwa wakilaani kwa kiasi
kikubwa kitendo hicho na kumwombea ili apone haraka.
“Tuseme kwa ufupi taarifa
ya Mhe Tundu Lissu imefunika kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya
habari”, imethibitika hivyo.
Mhe Tundu Lissu amesafirishwa
kupelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi usiku wa kuamkia leo kwa ndege
maalum ya kukodi, ambapo Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi
wa Upinzani Bungeni pamoja na mkewe Tundu Lissu pamaoja na viongozi wengine wa kambi
ya upinzani bungeni waliandamana katika msafara huo.
Wakati huo huo viongozi
wengi Serekalini, Bungeni na pamoja na watu mbalimbali wameonekana kuguswa sana
na tukio hili nakushiriki kikamilifu kumjulia hali Mhe Tundu Lissu mara alipofikishwa
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma hapo jana.
![]() |
Gari ya Mhe Tundu Lissi iliyoshambuliwa kwa risasi zaidi ya tano,na kumjerui vibaya. |
Japo viongozi wengi wa Serekali
kuwepo jijini Dar es Salaam kuhudhuria kukabidhiwa kwa ripoti ya Bunge ya
Uchunguzi wa Madini ya Tananate na Almasi, wengi wao walirejea mjini Dodoma
haraka ili kuwa kumjualia hali Mhe Tundu Lissu wakiongozwa na Spika wa Bunge
Mhe Job Ndugai.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu pamoja na Katibu Mkuu wake
Dkt Ulisubisya na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na madaktari wengine wote,
walishirikiana vizuri na kufanya kazi ya kumpatia matibabu ya awali Mhe Tudu
Lissu ili damu isivuje kwa wingi katika majeraha ya risasi na kuweza kuokoa
afya ya Mhe Tundu Lissu pindi alipofikisha hospitalini hapo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment