MTANGAZAJI WA TV AKERWA NA REFA, ASEMA NI AIBU KWA NCHI YA URUSI. - Mazengo360

Breaking

Thursday, 12 October 2017

MTANGAZAJI WA TV AKERWA NA REFA, ASEMA NI AIBU KWA NCHI YA URUSI.

MTANGAZAJI mmoja wa mpira nchini Urusi alikasirishwa na refa aliyekuwa akisimamia mechi moja na kuondoka katikati ya mechi hiyo na hivyo basi akawaacha watazamaji wakiangalia mchezo huo bila maelezo.

Uwanja wa Soka wa Klabu ya Torpedo Vladmir ya Urusi.

Wakati wa mechi hiyo kati ya klabu ya Urusi ya Torpedo Vladmir dhidi ya Tekstilshchik Ivanovo kipa wa Ivanovo alimuangusha mshambuliaji wa upinzani kulingana na kanda za video.

Wakati huo timu hizo mbili zilikuwa 1-1.

Na badala ya refa huyo kutoa adhabu ya mkwaju wa penalty, alitoa mkwaju wa adhabu nje ya eneo hatari na kusababisha malalamishi kutoka kwa mashabiki na watazamaji .

Hatua hiyo ilimkasirisha mtangazaji huyo na kuamua kusitisha matangazo aliyokuwa akitoa kulingana na ripoti za Pravda.

Na wakati mkwaju huo wa adhabu ulipopigwa mmoja wa walinzi waliunawa mpira na kuzua madai ya mkwaju mwengine wa penalti lakini refa aliwaambia wachezaji kuendelea na mchezo hatua iliyo mlazimu mtangazaji huyo kumshutumu vikali refa huyo.

Na baada ya shutuma hizo ambapo mtangazaji huyo alimtaja bwana Nikolsky kuwa ''aibu kubwa kwa soka ya Urusi '', aliinuka na kuondoka huku akisema tazameni mechi bila mtangazaji leo .

Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1-1.


MWISHO.

No comments:

Post a Comment