KWENYE
vyombo mbalimbali vya habari za mtandaoni hivi leo ipo taarifa kwamba yupo
Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Chang’ombe mkoani Dodoma amekuwa akigawa
viwanja kwa wanawake wenye maumbile fulani tuu, (wenye makalio makubwa) huu ni udhalilishaji kwa
wanawake.
Hii ni lugha ya kuudhi na
tena ni kwenda kinyume kabisa na maadili ya uandishi wa habari kwa kutumia
lugha zinazo udhi.
Wanawake ni kundi au jinsi
iliyoumbwa na aibu, vinginevyo tungetarajia kwa muda huu wawe wameshaa paaza
sauti zao kwa mamlaka husika ili kumchukulia hatua mwandishi au chombo hiki
kilichotumia lugha hii ya kuudhi kwa mama au dada zetu ambapo ni kumdhalilisha
mwanamke.
Ni wazi mtoa taarifa hii alikuwa na lengo zuri la kuibua uovu unaotendeka kwenye jamii, lakini hakuweza kupata maneno mazuri na ya staa yenye kuweza kufikisha ujumbe wake huu kwa jamii?
Pamoja na wanawake kuwa pia na haki ya kumiliki au kupatiwa ardhi na kuimiliki, je kuwa na maumbile kama
aliyoyataja mwandishi ni kosa?
Hebu chukulia mfano
angekuwa ni mama mzazi wako, au dada yako au shangazi, ulipozaliwa ukajikuta
umezaliwa na mwenye maumbile kama hayo na ameshamilikishwa kiwanja, utamkataa
au kumdhalilisha kwa vile tuu ameumbwa na maumbile hayo na kumilikishwa kiwanja?
Nadhani tufike mahali
turudi kwenye maadili ya uandishi inavyopasa ambapo jamii inatakiwa kuheshiamiana na
kustahimiliana katika mambo yote.
Cha ajabu hapa moja ya
mitando iliyo ripoti habari hiimmoja wapo ni chombo kinachoheshimika sana hapa
nchini, na hatuamini kama haina wahariri waliobobea katika lugha za kiuandishi zilizo na staa.
Ni vizuri mamlaka zinazo
husika zikemee na kuonya matumizi ya lugha za kuudhi na kudhalilisha kama hizi
kwa lengo tuu la kufikisha ujumbe husika kwa jamii.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment