WAINGEREZA WAMSHUKURU WAYNE ROONEY. - Mazengo360

Breaking

Wednesday, 23 August 2017

WAINGEREZA WAMSHUKURU WAYNE ROONEY.

WATU mbalimbali nchini Uingereza wanaojihusisha na mchezo wa soka wamempongeza nguli wa mchezo huo Wayne Rooney kwa kulitendea haki soka la Uingereza na kusema anastahili tuzo ya heshima.

Wayne Rooney akishangilia moja ya magoli aliyoifungia timu ya Taifa ya Uingereza, 

Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la “The Telegraph,” mwenyekiti wa FA, Greg Clark amemtaja Rooney kama alama ya Taifa la Uingereza katika soka na kuongeza kuwa alilitendea haki soka la Taifa hilo.
Wayne Roone, 31, ambae ametangaza kustaafu soka katika timu ya Taifa ya Uingereza ingali bado akiwa katika kiwango cha ujana wake baada ya kurejea katika timu yake ya Everton ambapo hadi anatanga kustaafu ameshaifungia club hiyo magoli mawili kwenye msimu huu wa ligi ya premier.

Wayne Rooney akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake ya Everton katika ligi ya Premier.

Nae mwandishi nguli wa habari za michezo nchini Uingereza Alan Tyers amemwagia sifa Rooney kwa umairi aliouonyesha wakati wa mchezo kwa kizazi chake, ambapo pamoja na nguli wengine Rooney aliweza kuiletea sifa Uingereza katika medani ya soka na sasa ameacha heshima kubwa.
Wengine aliocheza nae katika timu ya Taifa ya Uingereza ambao wote wameshastaafu soka ni pamoja na Owen, David Beckham, Stephen Gerald na Frank Lampard. Wengine ni Paul Scholes na Rio Fernandes.
Rooney alianza kuchezea timu ya Taifa ya Uingereza mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 18, nakufanikiwa kuisaidia Uingereza kuingia kwenye robo fainali ya Europian Championship.
Amestaafu soka kwenye timu ya Taifa ya Uingere akiwa na rekodi ya mabao 53 huku akishuka dimbani mara 119 akiwa na timu yake ya Taifa ya Uingereza.
(Taarifa na picha, kwa mujibu wa The Telegraph la Uingereza).

MWISHO.

No comments:

Post a Comment