WAZIRI wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kampuni
ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa jitihada
kubwa wanazozifanya katika kusimamia maadili kwa kuhabarisha na kuielimisha
jamii ya Kitanzania.
![]() |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji
Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Bw. Francis Nanai (kulia) wakiwaonyesha
Waandishi wa habari muonekano mpya wa gazeti la michezo la Mwanaspoti mara
baada ya uzinduzi Jijini Dar es Salaam.
Pongezi
hizo amezitoa jana wakati wa Uzinduzi wa Muonekano Mpya wa gazeti pendwa la
michezo la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni hiyo.
Dkt.
Mwakyembe amesema kuwa, mara kwa mara MCL imekuwa ikiisaidia jamii kwa
kujihusisha katika masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wakati wa tetemeko
la ardhi Mkoani Kagera imeweza kutoa mchango wake mkubwa kwa jamii na daima
imekuwa ikilinda maadili na weledi wa kazi ya uandishi kwa wafanyakazi wake
jambo ambalo linaonyesha ushirikiano mzuri baina ya Serikali, Kampuni na jamii.
“Mimi
nawapongeza na kuwashukuru sana MCL kwakuwa mstari wa mbele katika kulinda
maadili katika kazi zenu, endeleeni kulinda maadili kwa kuhabarisha na
kuielimisha jamii, sijaona mkivunja maadili ya kazi zenu na hakika mnajijengea
sifa nzuri kwa wengine”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliongeza
kuwa, kwa sasa kumeibuka wimbi kubwa la Waandishi wa habari (Makanjanja) ambao
hawana vyeti wala weledi wa kufanya kazi ya uandishi wa habari na hao wamekuwa
kila wakati wakirusha taarifa zisizo sahihi hususani katika mitandao ya kijamii
jambo ambalo Serikali haiwezi kulifumbia macho.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw. Francis Nanai amesema kwamba lengo
la kampuni hiyo kuja na muonekano mpya wa gazeti hilo ni kuwapa ladha mpya
wasomaji wake nchini kote, na hiyo ni mara ya sita kwa gazeti hilo kubadilishwa
muonekano wake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001.
“Sisi
kama wadau wa michezo tumewasikiliza wasomaji wa gazeti letu na tukayafanyia
kazi mawazo yao na ndiyo maana tukaamua kuja na muonekano mpya wa gazeti hili
ambao uko kimataifa zaidi”, alisema Nanai.
Aliongeza
kuwa, gazeti hilo lilianzishwa na waandishi wa tatu mwaka 2001 na lilikuwa
likitoa nakala 3,000 kwa siku ambapo kwa sasa kuja kwa muonekano mpya wa gazeti
hilo kutaongeza idadi ya wasomaji tofauti ilivyokuwa mwanzo na idadi ya
uchapishaji imeongezeka hadi kufikia nakala 60,000 kwa siku.
MWISHO
No comments:
Post a Comment