BIASHARA YA KUUZA MIILI YANYOOSHEWA KIDOLE. - Mazengo360

Breaking

Friday, 15 September 2017

BIASHARA YA KUUZA MIILI YANYOOSHEWA KIDOLE.

SEREKALI imesema, wanawake wanaoishi kwa kutegemea kipato cha kujiuza miili yao wanavunja sheria na ni kosa la jinai hivyo imetoa wito kwa jamii kuacha na kuepuka vitendo hivyo viovu na vyenye kudhalilisha utu wa mtu.

Baadhi ya akina mama wakiwa katika maeneo yao biashara.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala wakati akijibu swali bungeni.

Naibu Waziri amesema “kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai kifungu namba 176(A) kinaeleza ni kosa la jinai kwa mwanamke kutumia mwili wake kama bidhaa na kujipatia kipato cha kuendeleza maisha yake ya kila siku.”

Ametoa wito kwa jamii kuepuka matendo hayo maovu ya kimaadili na kueleza zaidi kwamba, serekali kupitia jeshi la polisi kote nchini inaendelea na zoezi la kuwabaini wote wanaofanya biashara hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wakiwamo wenye biashara za madanguro.

Siku za miaka ya hivi karibuni katika maeneo mengi ya mijini na hata vijijini kumezuka mtindo wa watu kufanya biashara za kuuza miili yao na kujipatia pesa kama jambo hilo si kosa, ambapo ni kinyume kabisa na utu wa mwanadamu, amefafanua zaidi Naibu Waziri.

Maeneo mengi katika miji mikubwa biashara ya ngono imeshamiri.

Aidha, maeneo yanayoongoza kwa mtindo huo ni ya kumbi za starehe, mabaa, stend za mabasi na hata maeneo ya mahoteli makubwa na mighahawa, ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakijitafutia na kuwanunua wanawake kama bidhaa na kustarehe nao kwa malipo maalum na kuongeza kwamba ni hatari kimaadili na hata kiafya, alisema.

Amewataka wanaume wote kuacha pia kutia chumvi katika biashara hiyo yaani kuwanunua akima mama kama bidhaa ili kusaidia kukomesha tabia hiyo mbaya inayokwenda kinyume na maadili ya mwafrika na mtanzania kwa ujumla, alimalizia Naibu Waziri. 
   

MWISHO.

No comments:

Post a Comment