MBARONI KUJIHUSISHA MAPENZI JINSIA MOJA. - Mazengo360

Breaking

Saturday, 16 September 2017

MBARONI KUJIHUSISHA MAPENZI JINSIA MOJA.

JESHI la Poisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya Jinsia moja katika ukumbi wa Hotel ya Masoon Shangani wakiwa kwenye mafunzo ya kuhamasishana juu ya vitendo hivyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharii, Hassan Nassir akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kukamatwa wanaotoa elimu juu mapenzi jinsia moja huko Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kufuatia tukio hilo huko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ya Mkoa huo Muembe Madema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Hassan Nassir amesema idadi ya waliokamatwa ni kumi na mbili kati yao wanawake ni wanane na wanaume wanne.

Kamanda Nassir amesema zaidi kwamba, Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa suala hilo sambamba na kuwachukulia hatua wahusika wa masuala hayo ambayo yanakiuka mila, silka, utamduni na desturi pamoja na maadili ya nchi yetu.

Hata hivyo, Kamanda Nassir amewataka wazazi na walezi kuwafuatilia na kuwa karibu na watoto wao na kuhakikisha hawajiingizi katika vitendo hivyo viovu ili kuokoa vizazi ambavyo ni tgemeo la Taifa letu.

Watu hao wamekamatwa wakiwa katika mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Bridge Organization iliyosajiliwa nchini kwa lengo la kutoa elimu ya maradhi ya ukimwi lakini imeenda kinyume na badala yake inajihusisha na kampeni ya kuhamasisha mapenzi ya Jinsia moja.

(Habari na picha kwa hisani ya mwandishi wetu Zanzibar)


MWISHO.

No comments:

Post a Comment