SEREKALI ya Tanzania imesema
itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kukuza lugha ya Kiswahili katika ukanda wa
nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa walimu wa lugha hiyo katika
mataifa mengine duniani.
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe Samia Suluhu Hassan akihutubia kongamno la kwanza la Kiswahili la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoanza leo mjini Zanzibar. |
Akihutubia wajumbe wa Kongamano la kwanza la Kiswahili la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suhulu Hassan amesemaKiswahili ndio nyenzomuhimu ya kuwaunganisha wote.
Mhe Samia aliendelea kusema zaidi kwamba, Tanzania itabakia kuwa msaraei wa mbele katika kukuza na kudumisha
Kiswahili katika Ukanda huu na kuongeza kwamba ipo tayari kutoa walimu wa
Kiswahili katika nchi majirani.
Pia Mhe Samia ameeleza kwamba, kufanyika kwa kongamano hilo lakwanza
la Kiswahili katika ukanda huu mjini Zanzibar
ni kuthamini mchango mkubwa wa lugha hiyo ambapo inafungamanishwa na umuhimu wa
kihistoria ambapo nimwanzo mzuri wa
Kamisheni ya Kiswahili katika kutekeleza kazi zake, alifafanua Makamu wa Rais.
Aidha, Mhe Samia ameeleza kwamba serikali za nchi wanachama wa jumuya ya Afrika mashariki zijitahidi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kuiwezesha kamisheni hii ya Kiswahili ili iweze kutekeleza mapendekezo ya kisera yatakayotolewa baada ya kongamano hilo.
Kongamano la kwanza la kamisheni ya kishwahili jumuiya ya Afrika
Mashariki litaendelea kwa mfululizo kwa siku mbili mjini Zanzibar ambapo limeshirikisha
jumla ya wajumbe zaidi 150 kutoka nchi za ukanda huu pamoja na wawakilishi wa
baadhi ya nchi nyingine barani Africa wakiwemo waadhiri wa vyuo vikuu na
waandishi mbalimbali wa habari.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment