KAMATI teule
ya bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai leo imewasilisha ripoti
zake mbili huku ikiwataja vigogo serikali kuhusika katika ufujaji mkubwa wa
madini ya Almasi.
![]() |
Mhe George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI nae ameguswa na ripoti ya Bunge kuhusu madini ya Almasi iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma. |
Ripoti hizo mbili zilizowasilishwa leo bungeni mjini Dodoma ziwataja baadhi ya mawaziri wa Nishati na Madini wa sasa na wa zamani kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kinachoaminika kuwa ni uzembe wa makusudi uliousababishia tena serikali hasara kubwa.
Waliotajwa katika ripoti
hizo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini Mhe William
Ngeleja na mwenzie aliyemfuatia ofisini aliyekumbwa na kashfa ya ESCROW na ile
ya makinikia ya ACACIA Mhe Prof Sospeter Muhongo.
Wengine wapya walioongezeka
katika orodha ya sasa ni pamoja na Mhe George Simbachawene, ambaye kwa sasa ni
Waziri wa TAMISEMI, ambaye pia alishawahi kuwa Waziri katika Wizara hiyo ya
Nishati na Madini pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMAA na Mwenyekiti WA Kamati Teule ya Rais ya kuchunguza
Makinikia ya ACACIA Prof Abdilkarim Mruma.
![]() |
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Musa Azzan Zungu. |
Pia wengine wamo Mhe Edward
Ngonyani pamoja na Mwanasheria aliyejiuzulu pia katika kashfa ya ESCROW Mhe Fredrick
Werema.
Katika kamati ya uchunguzi
wa Almasi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake Mhe Mussa Azzani Zungu (Mbunge wa
Ilala-CCM) kamati hiyo imeeleza kusikitishwa na kampuni ya uchimbaji wa almasi
kumzawadia kiongozi mmoja mkubwa ambaye alikuwa serikalini (Haikutaja jina) almasi
yenye thamani ya dola milioni 20.
Ripoti
hiyo pia imesema taratibu za uchimbaji wa almasi hapa nchini unafanywa kiholela
huku kampuni nyingi zikiwa vinara wa
kukwepa kulipa kodi serikalini kwa kubadilishana majina ya makapuni kwa madai ya
kusingizia kupata hasara ili kukwepa kodi, ripoti ilieleza.
Akizungumzia
kampuni ya uchimbaji wa madini ya Williamson Diamond, ripoti imesema tangu
mwaka 2007 hadi 2017 haijawai kulipa mapato yeyote serikalini kwa kulipa kodi.
Amesema
kuwa kuwa kampuni hiyo haikuweza kulipa kodi na Mrabaha kwa kisingizio kuwa
kampuni inapata hasara,huku ripoti hiyo
ikihoji kwamba kama kweli kampuni inapata hasara kwanini isitangaze
kufilisika nakuondoka.
Alisema
licha ya kuwa almasi ya Tanzania kuwa bora kuliko sehemu nyingine lakini bado
serikali imekuwa hainufaiki na jambo lolote kutokana na madini ya almasi.
![]() |
Waziri wa Zamani Mhe Prof Sospeter Muhongo. |
Kamati
ya Zungu imempata Prof.Mruma na hatia ya kuruhusu madini ya Almasi yapotee
kizembe wakati akiwa Mwenyekiti wa bodi ya uwakala wa ukaguzi wa madini
Tanzania (TMAA).
Zungu
alisema Profesa Mruma alipohojiwa aliiambia kamati kwamba alisaini bila kusoma
kwa undani nyaraka husika.
Alipoulizwa
kwanini alisaini bila kusoma, alisema alikuwa 'busy' sana na hivyo hakupata
muda wa kusoma nyaraka hizokwa kina na hivyo aliamua kusaini kwa kuwa amini
watendaji wa wizara waliokuwa chini yake.
Kamati
zote mbili zimempata Mhe George Simbachawene na hatia ya kusaini Mikataba yenye
madudu mengi yaliyoingiza nchi yenye kuleta hasara kubwa.
Simbachawene
ni moja wa watu ambao walisha wahi kufanya kazi Shirika la STAMICO.
Aidha
Zungu amesema kuwa Prof Muhongo nae alisaini mkataba wa Tanzanite na kampuni ya
TML licha ya kushauriwa na mwanasheria mkuu na mwanasheria wa wizara asisaini.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment