NAIBU Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana
nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya
malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri Wambura ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la Miss Garden Route 2017/2018 Mei 6 mwaka huu nchini humo katika mji wa George.
Mlimbwnde
Witness aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa
washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.
“Ni
dhahiri umetumia ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na
sheria ambavyo umevipata kutoka kwa familia, jamii ya Kitanzania na pia
kwa jamii ya watu wa Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.
“Vijana
wa Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la
Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili
kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.
Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.
Hatua
hiyo inaonesha Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali
kutumia muda wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake
la msingi nchini humo ni la Kimasomo.
Zaidi
ya hayo Naibu Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo
inatambulisha utamaduni, kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa
kuongeza juhudi, maarifa na kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta
matokeo mazuri yenye tija.
![]() |
Mshindi wa taji la
Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy
Kavumo.
|
Aidha, Naibu Waziri Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza kipato na kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake yeye binafsi na kwa Taifa.
Kwa
upande wake Miss Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa
anajivunia kuwa Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri
Watanzania kusimama kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea
maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Mashindano
ya Miss Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa
kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel
Bay Afrika Kusini.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment