Zaidi ya Watu 50 wakamatwa na Jeshi la Polisi Kigoma kwa tuhuma za Mauaji na kuharibu Mali kwa kuchoma Moto kijiji cha Kabanga. - Mazengo360

Wednesday, 6 September 2017

Zaidi ya Watu 50 wakamatwa na Jeshi la Polisi Kigoma kwa tuhuma za Mauaji na kuharibu Mali kwa kuchoma Moto kijiji cha Kabanga.

21390485_1597013813671856_1312721490_o

Pichani ni Mali mbalimbali zilizoteketezwa kwa Moto na Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kgoma.

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Songoye ameuawa kwa kuchomwa moto na Wananchi katika kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika tukio ambalo pia wameteketeza kwa moto nyumba saba, magari mawili, pikipiki nne na mali za familia za watu sita ambao wanawatuhumu kufanya mauaji ya watu kijijini hapo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikina ili watajirike.
21390288_1597013827005188_964334396_o

21392896_1597013780338526_583166557_o

21439499_1597013807005190_938432479_o
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Naibu Kamishna wa Polisi Ferdinand Mtuiamesema zaidi ya watu hamsini wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo lililotokea Jana September 4,2017 huku Kaimu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Marco Gaguti ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe akitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

21458686_1597013790338525_181098083_o