SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inandaa utaratibu
maalum kupitia Benki Kuu (BOT) wa kujua fedha zinazotumwa nchini upande
wa Zanzibar kutoka kwa wanadayaspora ili zichangie vya kutosha kuinua uchumi.
![]() |
Benki Kuu ya Tanzania (BOT). |
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kongomano la nne la watanzania wanaoshi nje ya nchi, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na Mwemyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu amesema azma ya serikali ni kuwashawishi wanadayaspora kuja kuwekeza nchini kwa ajili ya maslahi ya nchi yao na wao wenyewe.
Ameeleza zaidi kuwa uwepo wa wanadayaspora utaleta mafanikio ya
haraka katika sekta mbalimbali ikwemo
kusaidia katika nyanja za elimu na afya na kukuza zaidi ustawi wa taifa kiuchumi.
Aidha akizungumzia kuhusu suala la utakitishaji wa
fedha haramu kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi na wawekezaji, amesema
Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga vizuri katika
kukabiliana na tatizo hilo linaloisumbua dunia kwa hivi sasa, alifafanua zaidi.
Wakati huo huo Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar limesema
linajipanga kusogeza huduma zake jirani zaidi na wilaya zote za mjini na
vijijini ili kuwarahisishia wanafunzi na wananchi wote kupata fursa ya
kujisomea vitabu kwa urahisi.
Akizungumza na mwandishi wa habari Mkurugenzi wa Maktaba Zanzibar
Sichana Haji Fumu amesema wananchi wengi wanoishi katika maeneo ya mbali hasa
vijijini kwa kiasi kikubwa wanakosa upatikanaji wa elimu kwa njia
ya kujisomea vitabu kutokana na umbali na uhaba wa maktaba uliopo hivi sasa.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo ameeleza kwamba ongezeko la watumiaji
wa maktaba hususani kwa upande wa Pemba umeongezeka hivi sasa kutokana na uwepo
wa maktaba katika wilaya za Chake Chake, Wete na Wingwi.
Hivyo amewataka wananchi na wanafunzi kujenga utamaduni wa
kuzitumia makataba zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi na uelewa zaidi katika
maisha ya kila siku.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment