SERIKALI kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo imesema kuwa inakamilisha mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya
mwaka 1995 ili kuhakikisha inaendana na mahitaji ya sasa katika maendeleo ya
michezo nchini.
Hayo yamebainishwa
na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi aliyetaka
kujua mipango ya Serikali katika kufufua mchezo wa Riadha Bungeni Mjini Dodoma
leo.
“Serikali kwa
kushirikiana na wadau inatekeleza programu mbalimbali za kuendeleza mchezo wa riadha nchini ikiwemo Kilimanjaro
Marathon,Bagamoyo Marathon,Heart Marathon na Tulia Marathon ambayo hushirikisha
wanariadha kutoka nje”,Aliongeza Mhe.Wambura.
Aidha pamoja na hayo
Mhe.Wambura amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja na
Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendesha mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA ambayo pamoja na mambo mengine yanalenga
kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika mchezo wa riadha.
Akizungumzia suala
la miongozo ya Kiserikali amesema kuwa Wizara yake inakamilisha taratibu za
kuandaa miongozo ya kiserikali ili kuwezesha wadau wote kuendesha shughuli
zao katika mazingira ya weledi na stadi bora za michezo.
Hata hivyo Naibu
Waziri uyo amesema kuwa nchi yetu imeanza kufanya vizuri katika mashindano ya
Riadha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma kupitia kwa wanariadha wake kama
Francis Naal,Samson Ramadhani,Gidamis Shahanga,Juma Ikangaa,Suleiman Nyambui na
Filbert bayi na hivyo kuitangaza nchi yetu.
“Nchi yetu kwa sasa
imeanza kupata mafanikio katika riadha kupitia wanariadha wetu kama Alphonce
Simbu aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya standard Chartered
Mumbai Marathon,Cecilia Ginoka Panga aliyeshinda Beijing International Half
Marathon na Giniki Gisamoda aliyeshinda Shanghai International Half
Marathon,wote hawa wanaitangaza nchi yetu vizuri na kuifanya ifahamike na hivyo
kuvutia watalii ”Alisisitiza Mhe.Wambura.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment