FEDHA ZA ESCROW ZA MOTO KWA MHE NGELEJA. - Mazengo360

Monday, 10 July 2017

FEDHA ZA ESCROW ZA MOTO KWA MHE NGELEJA.

WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa sasa wa Sengerema (CCM), Mhe William Ngeleja amerejesha serikalini fedha za mgao wa Escrow Tshs 40.4 milioni hivi leo.

Ngeleja+3

Kulingana na taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam, Mhe Ngeleja amesema ameamua kufanya hivyo ili kulinda hadhi na heshima yake kwenye jamii.
Suala la fedha za akauti ya Escrow ni moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli imeamua kupambana nayo na hadi sasa wamiliki wa Kamapuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL ya Dar es Salaam ambao ni Harbinder Sethi Singh na James Rugamalira tayari wapo kizuizuini kwa tuhuma hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba, mnamo February 12, 2014 Bwana James Rugemalira ambae ni mmiliki wa kamapuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd alimpatia kiasi hicho Waziri huyo wa zamani fedha hizo kupitia benki ya Mkombozi ya jijini Dar es Salaam.
Ameeleza madhumuni ya fedha hizo ilikuwa zimsaidie kutekeleza majukumu yake ya kibunge kwenye jamii anayoiongoza yaani wananchi wa Jimbo la Sengerema bila kujua zilikuwa na harufu ya tuhuma za rushwa.
Pia, Mhe Ngeleja amesema katikataarifa yake kwamba ni jambo la kawaida wabunge kuomba misaada toka kwa wahisani mbalimbali wa ndani na nje ili kujipatia fedha za kusaidia mipango ya kijamii ambayo bajeti ya serikali haiweza kuijumuisha mfano ujenzi wa makanisa, misikiti na kusaidia malipo ya ada kwa wanafunzi wasio na wazazi au walezi.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema kwamba Mhe Ngeleja mnamo January 15, 2015 alilipia kama kodi kwa aijili ya pato la  fedha hizo kwa kiwango cha asilimia 30% ilivyo sheria  kwa Mamlaka wa Mapato nchini yaani TRA, amabpo alilipiakiasi cha Tshs 13.138 milioni, taarifa hiyo ilisema.
Tuhuma za wahusika wa akaunti ya Escrow kwa sasa wanatakiwa na vyombo vya serikali kutoa ushirikiano ili kuona jinsi walivyozipata fedha hizo na ikiwa wana hatia ama lah.

MWISHO.