“Upo usemi; wote wenye hofu ya
Mungu hufanikiwa.”
Ni kama weekend hii jiji la Dar es
Salaam lilitekwa kwa muda na mbabe wa muziki wa hip pop nchini, Joseph Haule
ambae pia ni Mbunge wa Mikumi (CHADEMA).
Profesa
Jay, alifunga ndoa na mchumba wake Grace waliochumbiana kwa muda mrefu
takribani miaka 13, kama vile alivyofanya mchezaji wa Barceloan, Messi amabe
pia majuzi alifanya kama Profesa Jay, walipofunga pingu za maisha pale kanisa
la Kuu la Cathedrali la Mt Joseph la Jimbo Kuu la Dar es Salaam hapo jana.
Kama
haikutosha, wakaamia ukumbi wa Mlimani City, baada ya kubebwa na magari ya
kijanja ya tena ya kisasa aina ya Range Rover mapyaaa na upya wake.
Huku
akisindikizwa na wapambe wake wabunge wa Ukawa, mijeda yote nguli tena wa nguvu
akina Peter Mhe Msigwa, Mhe Joseph Mbilinyi aka Sugu, na kiboko cha mzee wa
Kiraracha, Mhe Mbunge Mbatia nao walikuwepo.
Sasa
kule Mlimani City usipime.
DJ
Mkuu na kiongozi wa CHADEMA aka mhangawa uwekezaji Mhe Freeman Mbowe nae akatia
timu akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Mhe Mzee Lowasa ilivyo jadi yao.
Lilikuwa
bonge la movie, pale ambapo mfalme wa muziki wa kizazihiki hapa nchini, Diamond
Plantinum alipofanya vitu vyake live pale stajini Mlimani City, huku Mzee
Lowasa, M/k wa CHADEMA Mhe Mbowe na Mbunge Mbatia wakishuhudia kama majaji.
Inavyooneka
Diamond pia alitambulisha mtindo mpya wa uvaaji kwa vijana wa leowa jinsi ya kiume,
ambapo mtindo wa suruali aina ya “don't touch” au “mchinjo” umerudi rasmi
sokoni.
Diamond
akipigilia “kobazi” (open shoes) zake za kijanja akaonekana simple, ambapopia aliungwa
mkono pale stajini na mkali wingine anaetamba hivi sasa, Harmorraper nae
alitinga na “don't touch” yake kimtindo.
Akina
dada wa kibongo nao hawakubaki nyuma pamoja na vijana walipagawa na simu zao,
huku wakigombania kupata picha za kuuza sura na mfalme huyo wa muziki hapa
nchini Diamond Plantinum.
Professa
Jay, nae hakubaki nyuma.
Alijimwaga
stajini kucheza ngoma mpya ya Diamond akiwa na mahabuba wake Grace, huku
akishikilia mkia wa gauni lake lisiburuze chini la rangi ya dhahabu ya kung’aa.
Katika
dansi hilo kakaaa, zilipigwa ngoma za kijanja toka majuu zilizobamba miaka ya
nyuma.
DJ
Mkuu Mhe Mbowe, pamoja na kijana wa Arusha mjini Mhe Mbunge Lema na mkewe,
pamoja na Mhe Mbatia pia na mkewe waliyarudi kisawasawa mangoma ya kijanja na
kuendana kabisa na mdundo unayopigwa zaidi kule Uingereza katika Ukumbi wa
Etihad pale Machester City.
Wakali
hawa walinikumbusha enzi zetu miaka ya 80 na 90 tulipokuwa tukisoma shule za
bodini za sekondari, enzi hizo kwa hela yakahawa miziki hiyo tuliicheza sana
hadi tulikuwa tukitoroka shule na kwenda kwenye muziki.
Kipindi
hicho shule za Kibohehe, Mawenzi, Namfua, Kilimanjaro na zingine za mkoani Kilimnjaro
miaka hiyo, wacha kabisa.
Kiukweli
weekend hii Professa Jay na mkewe Grace ndio habari ya mjini.
Nahisi
bajeti nzima ya harusi hiyo sijui ilikuwa kiasi gani,kwani sijaona popote mambo
yalifanyika kishamba,hata kidogo.
TUNA WATAKIA WAWILI HAO, JOSEPH
NA GRACE MAISHA MEMA NA YENYE BARAKA TELE. MUNGU IBARIKI NDOA YAO.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment