MTANZANIA
anaecheza soka ligi ya Ujermani katika klabu ya RB Leipzing, Yussuf Poulsen
ameshauri watazania waheshimu thamani ya muda kama wanataka kufikia maendeleo wanayo
yatamani.
Yussuf mwenye umri wa miaka
23 na mwenye asili ya baba ambae ni mtazania kutokea jijini Tanga na kuzaliwa
na mama mwenye asili ya Denmark, ameitembelea Tanzania hivi karibuni na
kuhojiwa na mtandao wa kijamii wa Ayo Tv na kutoa ushauri huo.
Mtandao huo wa Ayo Tv
ulimfanyia mahojiano maalum mtazania huyo, ikiwamo sababu za kuchezea soka lake
kama mchezaji wa timu ya Taifa ya Denmark badala ya timu ya Taifa ya Tanzania,
alisema hajawahi kuombwa kufanya hivyo na vyombo husika toka Tanzania.
Alipoulizwa ni jambo gani
baada ya kufika nchini lililo mshangaza sana na pia ni kitu gani anachoshauri
wachezaji wa kitanzania ili waweze kufikia mafanikio kama aliyonayo hivi sasa,
Yussuf alieleza kwamba,
“Ninashangazwa sana jinsi
watanzania wasivyo zingatia thamani ya muda,” alieleza mshambuliaji huyo wa RB
Leipzing ya Ujermani na mchezaji wa timu ya Taifa ya Denmark.
Alitoa mfano wa wazi
kwamba, mtu anaweza kupokea mwaliko wa kukutana na mtu mwingine au hata kufanya
mahojiano na mtu mwingine kwa muda fulani waliokubaliana, lakini cha kushangaza
muhusika badala ya kufika eneo husika nusu saa au robo saa kabla ili kuwahi
muda, yeye hufika nusu saa au saa moja baadae, kitu alichoeleza kwamba sio
kujali thamani ya muda.
Yussuf alitoa mfano toka
nchini Ujermani na Denmark kwamba suala la kuzingatia muda ni jambo la kisheria
na pia linachukuliwa kama ni jadi ambapo yeyote anaechezea muda au kutozingatia
muda, huweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amewataka watanzania
kuzingatia zaidi thamani ya muda na pia ametoa ushauri kwa wachezaji wa
kitanzania kujitoa sadaka na kuachana na mambo mengine na kufanya jitihada na
bidii zaidi kama wanataka kufikia mafanikio.
“Wachezaji wa kitanzania ni
vyema mkazingatia suala la muda na pia mjitoe sadaka kutumikia soka, endapo
mnataka kufikia mafanikio,” alishauri zaidi Yussuf.
(Taarifa na picha kwa
hisani ya Millard Ayo Tv na mitandao wa wikipedia) .
MWISHO.
No comments:
Post a Comment