CHAMA
cha wafugaji nchini (CCWT) wamekutana mjini Dodoma hapo jana kujadili namna ya
kubadilisha ufugaji wao ili uendane na sera ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya
uchumi wa viwanda.
Akitoa taarifa ya mkutano
huo mbele ya waandishi wa habari, mratibu wa mkutano huo ambae pia ni Katibu wa
Chama hicho Kanda ya Kati Bi Neema Ally alisema lengo kuu ni kujadili na
kutathmini ushauri wa Mhe Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan alioutoa kwa
wafugaji alipokuwa mjini Arusha mwezi uliopita juu yaufugaji unaoendana na sera
ya serikali ya uchumi wa viwanda.
Pia, alieleza kwamba
kulingana na hotuba aliyoitoa Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa
akihairisha Bunge jumalililopita mjini Dodoma, aliwashauri wafugaji kuandaa
mpango wa ufugaji wenye tija ili serikali iweze kuwasaidia kuwapatiamaeneo ya malisho
na mipango mingine.
Mkutano huo uliwakilishwa
na wenyeviti wa kanda wa wilaya na Kanda zote saba hapa nchini, ikiwamo Kanda
ya Kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, Kanda ya Ziwa yenye mikoa
ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Mara na Geita.
Kanda zingine ni ya
Magharabi yenye mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi na Bukoba na Kanda ya Mashariki
ambayo ni Dar Es Salaam, Pwani, Mtwara, na Lindi.
Alitaja pia Kanda zilizohudhuria
ikiwamo Kanda Kaskazini yenye mikoa ya Tanga,
Kilimanajoro, Arusha na Manyara pamoja na ile ya Nyanda za juu Kusini ya mikoa
ya Iringa, Njombe, Mbeya na Sumbawanga.
Akitoa mada katika mkutano
huo, mwakilishi toka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambae pia ni Afisa
Mifugo Mkuu wa Wizara, Bwana Simon Lyimo aliwaambia wafugaji hao kwamba, ni
vizuri kutambua mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri ufugaji na kuwataka
wabadilike.
Nae Mkurugenzi Mwendeshaji
wa Kampuni ya “Tanzania Livestock Product Ltd, Ernest Tarimo inayojishughulisha
na uongezaji thamani ya bidhaa zitokanazo na mifugo zikiwamo nyama, maziwa na
ngozi aliwashauri wafugaji hao juu ya kuunda mfumo madhubuti wa uongozi ili
hoja yao ya kutaka kuanzisha kamapuni ya kusindika nyama nchini iweze kufanyiwa
kazi na serikalikwa urahisi zaidi.
![]() |
Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Bwana Magembe Makoe akisoma mapaazio ya kikao mbele ya washiriki (hawapo pichani) katika mkutano wa wafugaji iliofanyika Dodoma hapo jana. |
Alieleza zaidi Mkurugenzi huyo kwamba, ili wafugaji waendane na sera ya serikali ya ujenzi wa viwanda, wafugaji lazima wajadili njia ya kupata mtaji wa shilingi bilioni 50, unaotakiwa katika mapendekezo ya kuanzisha kampuni ya kusindika nyama na mazao mengine ya mifugo kwa njia ya uuzaji wa hisa.
Amewataka pia waachane na
ufugaji wa kizamani kwani malisho kwa sasa ni shida na pia wasibakie kupishana
na serikali kugombania malisho na badala yake watumie ushauri wa wataalam
katika kufanya ufugaji bora na wenye tija.
![]() |
Washiriki ambao ni wafugaji toka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa wafugaji uliofanyika mjini Dodoma kujadili uchumi wa viwanda hapo jana. |
Mkutano huo wa siku moja
ulipitia na kupitia pia maazimio ya taarifa ya wafugaji itakayowasilishwa kwa
majadiliano ya pamoja kati ya uongozi wa CCWT na ofisi ya Waziri Mkuu baadae
mwezi huu, kufuatia hoja ya Mhe Kassim Majaliwa alivyowashauri.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment