HALMASHAURI
nchini
zimetakiwa kutumia vyema fedha zinazotengwa kwa ajili ya kundi la vijana na
wanawake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya
Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Kati na Viwanda.
Hayo yamebainishwa
leo na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam alipotembelea Maonesho ya 41 ya
Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) mabapo katika ziara hiyo aliambatana
na Mstahiuki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Benjamin Sitta.
“Taasisi za kifedha
zinao wajibu mkubwa katika kufikia adhima hii ya Serikali, lakini sisi Serikali
za mitaa, Halmashauri ziano wajibu mkubwa kuhakikisha zilie asilimia tano za
vijana na tano za wanawake zinakuwa sehemu ya kuchochea ufanikishaji wa dhamira
njema ya Serikali,” alisema Mhe. Mwita.
Aidha Mhe. Mwita ametoa pongezi kwa uongozi wa Tantrade kutokana na jitihada zao za kuhakikisha wanasaidia ukuaji wa bidhaa za ndani hasa bidhaa za ngozi ambapo alisisitiza ni vyema wakaendelea kuweka mkazo katika eneo hilo kabla ya kuangalia maeneo mengine.
Kwa upande wake Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta amesema kuwa Maonesho hayo ya
Sabababa yamekuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wengi na hata kwa wananchi
kuja kujifunza.
Aliongeza kuwa pamoja na wananchi kuja kujifunza lakini pia imekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mahusiano na wafanyabiashara wenzao kutoka nchi nyingine jambo ambalo katika biashara ni muhimu sana.
Nae, Kaimu Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin Ratageruka amesema
kuwa dhamira yake ni kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na soko la uhakika
ndani na nchi ya nchi.
Ameongeza kuwa kwa
kuanzia wamejikita zaidi katika bidhaa za ngozi ikiwa ni njia pia ya kuwainua
wafugaji ambao mazao ya mifugo yao yanatumika katika kutengeneza bidhaa
mbalimbali za ngozi.
“Serikali inatambua umuhimu wa kuthamini
bidhaa za ndani, ndiyo sababu Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu zoezi ambalo jumla
ya vijana 1000 walipatiwa mafunzo ya usindikaji na ushonaji wa ngozi, katika
mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam tawi la Mwanza,”
alisema Rutageruka.
Rutageruka ameongeza
kuwa katika kuendeleza jitihada hizo Gereza la Karanga (Moshi) na Kampuni ya
Woisso ya Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha viwanda kwa ajili ya
kutengeneza sole ili kuachana na utaratibu wa kuagiza skutoka nje.
Maonesho ya 41 ya
Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanafanyika huku azma ya Serikali ya Awamu
ya Tano ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati na
viwanda, kutokana na dhamira hiyo maonesho haya yamepewa kauli mibu isemayo;
“Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda.”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment