WATOTO
wawili wa uzao wa mkwewe Malkia wa Uingereza, Princess Dianah aliyefariki
August 31, 1997 wamedhamiria kumuenzi ipasavyo mama yao baadae mwezi ujao kwa kutimiza
miaka 20 tangu kifo hicho.
Kulingana na maelezo ya gazeti
leo la Uingereza la “The Dailymail” limeeleza, watoto hao ambao ni Prince
William na Prince Harry watafanya hivyo baadae mwezi ujao kwa kuandaa kipindi
maalum cha mahojiano ya Television ya ITV ya Uingereza.
![]() |
Princess Dianah akiwa na wanae kabla ya kifa chake August 31, 1997 |
Prince Harry amesema
kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa wao wawili kufanya hivyo tangu mama yao
alipofariki mnamo August 31, 1997.
Ameeleza pia kwamba,
kutokana na hali ya ujana uliokuwa ukiwakabili vijana hao hapo mwanzo,
hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo mapema, lakini kwa sasa wamekuwa watu wazima
hivyo wametambua umuhimu wa kumuenzi mama yao inavyo stahili.
![]() |
Prince Harry, kwa sasa umri wa miaka 32. |
Pia amesema kwamba, wanatambua mama yao alikuwa mama bora kwao na tena mwenye mapenzi ya dhati kwao kushinda vitu vyote duniani, hivyo na wao wata muenzi ipasavyo”, alifafanua Prince Harry.
Amemalizia kwa kusema zaidi
kwamba, katika mahojiano hayo na Television ya ITV ya kwamba, wataonyesha kwa
uwazi mahusiano yaliyopo kati yao na mama yao Princess Dianah na pia wataelezea
hisia zao zinavyoguswa na historia ya mama yao.
![]() |
Prince William. |
Pincess Dianah alikuwa
kipenzi cha watu, hususani alivyo jihusisha na masuala ya kijamii ikiwamo tasnia
ya urembo na kugusa mioyo ya watu wengi.
Wakati wa kifo chake
alimwacha Prince Harry akiwa naumri wa miaka 12 tuu, kifo kilichoamsha hisia
kubwa kwa watu hadi leo, ingali bado anaishi katika mioyo ya watu wengi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment