ILIKUWA siku ya
sikuku ya Noel au Christmas mnamo mwaka 1971. Mkuu mpya wa Mkoa wa IRINGA aliye
hamishiwa hapo akitokea Mtwara Dr. Wilbert Kleruu, msomi wa shahada ya uzamivu
wa uchumi wa kijamaa katika kilimo.
Kipindi hicho Kulikuwa na kampeni ya
kutaifisha mashamba ya wakulima wakubwa na kuyafanya mashamba ya kijiji. Na Dr
Kleruu alipelekwa Iringa ili akatekeleze kaz hiyo kwani kipindi hicho iringa
ilikuwa na wafanya biashara wakubwa walio miliki mashamba makubwa ya kilimo
hasa maeneo ya Isimani.
Katika Eneo hilo la Isimani Kulikuwa
na mkulima mmoja aliye kuwa ana miliki Takribani hekari 400 za mashamba na
mfanyabiashara aliye kuwa ana miliki majumba iringa mjini - Said Mwamwindi.
Kwa wakati, ule ilishauriwa angalau
kila mtu awe na shamba lisilo zidi hekari 4. Jambo ambalo lilileta mvutano
Mkubwa kati ya wakulima wakubwa na Serikali.
Sasa siku hiyo ya Christmas Dr.
Kleruu alikwenda Isimani akiwa katika utekelezaji wa sera ya kutaifisha
mashamba. Moja kwa moja alikwenda hadi shambani kwa Mwamwindi, na kumkuta
analima.
Mkuu wa Mkoa akamuuliza mbona
unalima shamba lako mwenyewe na si la kijiji? Mwamwindi akajibu, sioni tatizo
hakuna mtu shamba ni, Leo ni jumapli tena ni sikuku
Maneno Yale yalimuudhi Dr Kleruu,
ambaye alikuwa akisifika kwa ukali, kutekeleza sera za serikali, na maneno
makali au kutukana watu hadharani pale wanapo fanya makosa.
Dr. Kleruu baada ya kuudhika
alimtukana Mwamwindi tusi lililo mlenga mama yake ambaye tayari alikuwa amesha
kufariki siku nyingi.
Mwamwindi alihoji inakuwaje ana
mtukania mama yake, huku akimuonyesha kaburi alimo zikwa.
Mkuu wa Mkoa, aliendelea kuja juu,
huku akisema kaburi ndio nini? Huku akilipiga mateke kaburi la Mama yake
Mwamwindi.
Na ifahamike kwa kabila la wahehe
makaburini yana heshima yake, Kwani ndipo nyakati nyingine hutumika katika
Sala, matambiko na mila kadha,.
Kitendo kile kilimgadhabisha
Mwamwindi, na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani. Mkuu wa Mkoa akadhani
Mwamwindi ana mkimbia, akaamua kumfuata hadi nyumbani.
Alipo fika nyumbani, tayari
Mwamwindi alisha ingia ndani na kuchukua bunduki yake, Dr. Kleruu baada ya
kuona hali ile mara moja alianza kumuomba msamaha, Lakini hasira
zilimuwaka Mwamwindi kama moto wa nyika, hakuwa na msamaha, alimfyetulia
risasi Dr Kleruu na kumuua
Baada ya kumuua, Mwamwindi
aliuchukua mwili ya Mkuu w mkoa na kuuweka ndani y gari (seat ya nyuma) alilo
kuja nalo Mkuu huyo wa Mkoa, gari aina ya Peugeot.
Baada ya hapo alichukua kofia ya Dr
Kleruu na kuivaa, kisha akiingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea
iringa mjini. Tena akipita njia isiyo ruhusiwa kwani barabara ilikuwa 'one way'
Alipo karibia mjini, Askari
walishangaa ni nani anaye pita njia isiyo ruhusiwa, ila mara waligundua ilikuwa
gari y RC wa iringa, hivyo walidhani amepata dharura.
Gari ilipo wasilini kituoni, polisi
walijiandaa kupiga salute, mara alishuka Mwamwindi akiwa na bunduki yake na
kuelekea ndani (counter). Askari walipigwa na butwaa.
Alipo fika aliwaambia "nendeni
mkachukue Nguruwe wenu ndani y gari," na Kisha akakabidhi bunduki yake.
Lilikuwa tukio la kuajabisha, na
kushangaza na lililo fanyika kwa haraka sana.
Baada ya taarifa kuenea, msako wa
polisi ulianza mara moja. Msiba wa Dr. Kleruu ulikuwa pigo kwa wakulima
wadogo,walio sikitika kwa kifo hicho.
Ila katika msako huo, polisi
waliwakamata baadhi ya watu walio kuwa wakinywa bia kwa furaha, shangwe
na nderemo baada ya kusikia Dr Kleruu ameuawa. Kwani wanadai
alikuwa na dharau,.
Kesi ya Mwamwindi alipelekwa haraka
sana,. Na ndani ya miezi kadhaa, June 1972, Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa
hadi kufa, ikiwa ni moja ya hukumu chache za kunyongwa zilizo wahi
kuidhinishwa. Huo ndio ukawa mwisho wa tajiri na mkulima mkubwa, Saidi
Mwamwindi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment