WANAFUNZI wa
kike wilayani Kongwa mkoani Dodoma wameiomba jamii kutoa fursa zaidi kwao
kushiriki katika masuala ya uongozi katika jamii ili wajenge uzoefu zaidi na
kuwawezesha ushiriki ujenzi uchumi wa viwanda nchini kama viongozi watarajiwa.
Ushauri huo umetolewa na
mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Kongwa ijulikanayo kwa jina la St Francis Secondary, Magreth Lawrence, mwenye
umri wa miaka 16, wakati alipopatiwa nafasi ya kukaimu nafasi ya ukurugenzi wa
Halmshauri ya wilaya ya Kongwa na kuongoza kikao cha manejimenti ya halmashauri hiyo hivi
leo.
Tukio hilo ambalo ni sehemu
ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yanayoadhimishwa
kila mwaka October 11, liliandaliwa kwa pamoja kati ya uongozi wa Halshauri ya
Kongwa kwa kushirikiana na Shirika
lisilo la kiserekali la Plan International mkoani Dodoma.
Mwanafunzi huyo ambaye
alikaimu ukurugenzi wa halmashauri hiyo na kuongoza mkutano wa kawaida wa
menejimenti uliowashirikisha wakuu wa Idara na vitengo vya halmashauri hiyo,
kwamba endapo jamii itawapa fursa za kutoshakushiriki katika nafasi mbalimbali
za uongozi hapa nchini, wataweza.
Aliwaambia pia kwamba,taifa
kwa sasa linatekeleza sera ya uchumi wa viwanda na wao kama sehemu ya jamii ya
kitanzania wangependa wajenge uzoefu wa uongozi ingali bado vijana ili baadae
washiriki katika uongozi wa uchumi huo.
Nae Afisa Maendeleo ya
Jamii wa wilaya ya Kongwa Faraja Kasuwi ameeleza kwamba, Idara yake
ikishirikiana na halmashauri nzima ya Kongwa imejiwekea mpango mkakati wa
kuwawezesha watoto wa kike kujijengea uwezo wa kiuongozi katika jamii kwa
kuwapatia fursa mbalimbali kama hizo ili kujenga uzoefu wa uongozi.
Afisa Maendeleo huyo wa jamii pia ametoa wito kwa jamii nzima hususani katika mkoa wa Dodoma kubadilika na kuwa tayari kuongozwa na viongozi vijana ambao ni wanawake kwani wanao uwezo mkubwa sawa na wenzio wa jinsi ya kiume.
Ameongeza piakwamba,
wanatambua mila nyingi za kiafrika zilikuwa zikiwatenga watoto wa kike hususani
kupata na kutumia fursa za masomo hadi ngazi za juu na kuwanyima haki ya
kushiriki katika uongozi, lakini amesema kwamba wanaendelea kutoa elimu ya wao
kubadilika na kuwa tayari kuongozwa na viongozi vijana jinsi ya kike.
Maadhimisho hayo ya siku
yamtoto wa kike duniani kitaifa yanafanyika mkoani Mara na kaulimbiu ya mwaka
huu ni “tokomeza mimba za utotoni, tufikie uchumi wa viwanda”.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment