PHILIP MULRYNE ambae
alikuwa mcheza soko katika club ya Manchester United ya Uingereza ambae aliichezea
ligi ya Premier hapo siku za nyuma ametawazwa kuwa Padre wa madhehebu ya
Kikatoliki huko Ireland.
![]() |
Padre Philip Mulryne akiwekewa mikono na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dublin Joseph Augustine Di Moia huko Ireland juma lililopita na kuwa kasisi (Padre) wa Kikatoliki rasmi. |
Mcheza soka huyo, mnamo tarehe Julai
08, 2017 alitunukiwa wadhifa huo kwa mamlaka ya sheria za Kanisa Katoliki Dunia
huko Northern Ireland chini ya Shirika la Wadomisiani (Domician Order).
Mwanasoka huyo ambae kwa sasa
anajulikana kwa cheo cha Father Mulryne, inaripotiwa alikuwa akilipwa kitita cha Euro 600,000 kwa
mwaka wakati akiichezea Manchester United ya Uingereza.
Father Mulryne amepewa daraja hilo la
upadre na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dublin Joseph Augustine Di Moia ambaye alisafiri
kutoka Roma kwa ajili hiyo.
Father Mulryne aliweka nadhiri za kuishi
maisha ya kitawa na kutunukiwa pia daraja
la Ushemasi kulingana na taratibu za kanisa Katoliki mnamo Oktoba mwaka jana 2016.
Katika maisha yake ya ujana katika michezo,
Father Mulryne alifanikiwa kujiunga na timu ya Manchester United mwaka
1997 baada ya kuonesha kipaji katika timu za vijana na pia kuichezea timu ya
Taifa ya Northern Ireland.
![]() |
Padre Philip Mulryne enzi zake akisakata soka katika timu yake ya Taifa ya Ireland. |
Aliachana na Soka rasmi mwaka 2009 na akaanza safari yake ya kuelekea wito wa upadre na akajiunga na malezi ya Seminari ilivyo desturi.
Miaka miwili alisoma masomo ya
Falsafa katika Chuo cha Queen's University cha Belfast na Maryvale Institute
kabla ya kujiunga na masomo ya Theolojia katika Chuo cha Pontifical Irish
College na baade Chuo Kikuu cha Gregorian huko Italia.
Kulingana na taratibu za Kanisa
Katoliki, hua linautaratibu wa kuwapata vijana wenye vipaji mbalimbali vya hali
ya juu kadiri walivyozaliwa navyo ili waweze kusaidia jamii kubadilika na
kuishi maisha mema wakati wa utumishi wao katika jamii.
(Taarifa hii na picha kwa hisani ya BBC)
MWISHO.
No comments:
Post a Comment