![]() |
Katibu Mkuu Utumishi Dkt Laurian Ndumbaro. |
WIZARA ya
Utumishi wa Umma leo imetoa waraka mpya kuhusu wale ambao hawajawasilisha vyeti
vya kuhitimu kidato cha Nne na Sita ili vihakikiwe na baraza la mitihani laTaifa
wasimamishiwe mishahara yao kunzia mwezi huu wa July.
Kulingana na waraka
uliotolewa hivi punde leo jioni toka Ofisi ya Katibu Mkuu Utumishi mjini Dodoma
kwenda kwenye vyombo vya habari, umewaagiza waajiri wote nchini katika sekta ya
umma nchini, kutekeleza mara moja agizo hilo.
Waraka huo umeeleza bayana
juu ya mwongozo wa waraka wa serikali kwa watumishi wa umma no. 1 wa mwaka
2004, ambapo ulieleza utaratibu wa ajira serikali na kutaja kiwango cha chini
cha elimu ni kidato cha nne.
Kwa maelekezo haya
yakusimamisha mishahara ya wale wote ambao vyeti havijawasilishwa kwa uhakiki,
ina maana kusimamishwa ajira hadi hapo taarifa zao zitakapothibitishwa kuwa
zipo sahihi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment