![]() |
Upimaji naUshauri ukutolewa na wataalam wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwenye maonyesho ya 77jijini Dar. |
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete imewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao hasa magonjwa ya moyo katika msimu huu wa maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika viwanja vya maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kumekuwa
na muitikio mkubwa sana kwa wananchi kutembelea banda lao ambapo amesema kuwa kwa
siku takribani watu 700 wanafika katika banda hilo kwa ajili ya kupata huduma
na ushauri.
“Ni
vizuri watanzania wakatumia fursa hii kufika hapa na watapatiwa baadhi ya vipimo na
ushauri bure katika banda letu lililopo ndani ya viwanja vya sabasaba kwa
kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi wake kwa
kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote za msingi zenye kiwango na ubora,” Alisisitiza
Prof. Janabi
Akifafanua Prof. Janabi amesema Taasisi hiyo imedhamiria kuwahudumia wananchi
wakati wote wa maonesho na hata baada ya hapo wapo tayari kuwahudumia wale
wanaohitaji huduma katika taasisi hiyo.
Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa ikitoa huduma za upasuaji wa moyo tangu
kuanzishwa kwake hali inayosaidia kupunguza gharama zilizokuwa zinatumika
kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa kipindi kirefu sasa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment