ZIARA ya
Rais Mstaafu wa Ireland pamoja na mwenziwe Graca Machel wamelipongeza Bunge la Tanzania kwa kufanya
jitihada za kutosha kutunga sheria zinazo lenga kutunza afya ya jamii wakiwamo
wazee, akina mama na watoto.
![]() |
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Job Ndugai (kulia) akimkabidhi Rais Mstaafu wa Ireland Bi Mary Robson picha ya jengo la ofisi ya Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma hapo jana. |
Ugeni huo uliomtembelea
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ofisini kwake hapo jana mjini Dodoma, walieleza
jinsi walifurahishwa na hatua serikali ya Tanzania ilizofikia pamoja na Bunge
la Tanzania wanavyo shirikiana kutekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu
afya ya jamii, japo zipo changamoto.
Rais huyo mstaafu wa
Ireland Bi Mary Robson na Bi Graca Machel kwa nyakati tofauti wakati wa
mazungumzo yao na Spika, walieleza jinsi walivyofurahishwa na ziara yao hapa nchini
na kuzuri pia mkoa wa Dodoma ikiwamo wilaya ya Bahi na kusema wameridhishwa na
jitihada zilizoonyeshwa.
![]() |
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Bi Graca Machel kwa makini hapo jana baada ya ugeni huo kumtembelea ofisini kwake. Katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland Bi Mary Robson. |
Bi Graca Machel yeye alisema,
malengo ya ziara hiyo ni kujionea jinsi serikali ya Tanzania na vyombo vyake
ikiwamo Bunge inavyotekeleza utoaji huduma kwa wazee, ambapo wao ni wadau
wakubwa katikampango huo hususani afya za wazee.
Bi Graca Machel alimshauri
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai na Bunge pamoja na serekali kwa ujumla,
wasiridhike na hatua iliyofikiwa hadi sasa bali waendelee na jitihada hususani
katika kutunga sheria zitakazowezesha mazingira rafiki yakayotoa fursa zaidi
katika kutoa huduma ya afya kwa akina mama, watoto na wazee.
Nae Spika wa Bunge Mhe Job
Ndugai alipokea salamu hizo za pongezi toka kwa viongozi hao na kuahidi
kuendelea kuandaa sheria zenye kuleta mafanikio zaidi katika sekta ya afya hapa
nchini.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment