TANZANIA inaingia tena
kwenye vitabu vya historia na maajabu, baada ya kwenye moja ya mbuga za utalii
nchini kuonekana Simba akimyonyesha
mwana chui.
Wawili hao walikutwa na mtalii Joop
Van Der Linde mgeni katika eneo la utalii la Ndutu Safari Lodge hapa nchini
katika eneo la uhifadhi la wanyama pori huko Ngorongoro.
Limekuwa tukio la ajabu kwa sababu
ya utofauti wa jamii ya wanyama hawa, Simba akitokea jamii ya Leo na Chui
akitokea jamii ya Tigris. Wote wakiwa ni Panthera.
Eneo hilo ni la ukanda wa Serengeti
ambapo Simba huyo amepewa jina Nosikitok na ana umri wa miaka mitano.
Wahifadhikatika porihilo amewekewa Simba
huyo mfumo wa GPS katika shingo yake ili kufuatiliakwa karibu zaidi tabia zake.
Kwa msaada wa chombo hicho Simba huyo amegundulika kuwa na
watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28, mwaka huu.
(Chanzo:
BBC SWAHILI na Picha kwa hisani ya Joop Van Der Linde/ Ndutu Safari Lodge).
MWISHO.
No comments:
Post a Comment