NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Selemani
Jafo(Mb) amelipongeza Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa(UN-Habitat)
kwa kuanzisha ushirikiano na Serikali kwa kuweka mpango wa kuboresha Miji endelevu
Mkoa wa Dodoma.
![]() |
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe Seleman Jafo. |
Mhe Jafo aliyasema hayo mjini Dodoma
mwishoni mwa juma lililopita alipokuwa akifunga warsha iliyowashirikisha
waataalam wa makazi toka Shirika la Umoja wa Taifa na Mamlaka ya mafunzo ya
Ufundi nchini (VETA) kupitia wizara ya TAMISEMI.
Mhe.Seleman Jafo amewataka wataalam
kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kushirikiana kikamilifu na wadau mbalimbali
ambao wanataka kuleta maendeleo mjini Dodoma kwa kuwa serikali ya sasa
inahitaji mpango shirikishi kwa wataalam wetu na kwa wananchi kwa ujumla.
Mhe Jafo alitoa wito kwa watendaji
katika sekta inayojishughulisha na ustawishaji wa miji na makazi kutilia
umuhimu wa kupanga vizuri miji midogo hususani ile inayozunguka mji wa Dodoma baada
ya serekali kuhamishia shughuli zake toka Dar kuja Dodoma, ili iwe kivutio cha
utalii na biashara hapo baadae.
Ameshauri miji yote inayozunguka mkoa wa Dodoma ni vizuri ikafanyiwe tathmini nzuri na ipangwe kwa lengo la kuvutia utalii na si kuiacha ikue kihole kama inavyofanyika hivi sasa, alisema.
“Miji midogo iliyopo pembezoni mwa
mkoa wa Dodoma inakuwa kwa mfano Chemba, Bahi, Kibaigwa ambayo inakuwa
pasipo kuwa na mpangilio mzuri ni wakati wa wataalam waliopata mafunzo haya
kutoa ushirikiano katika kuboresha makazi yao ili yawe ya kisasa na endelevu na
kuwa kivutio kwa wageni wanaokuja” alisema Mhe Jafo.
Mhe Jafo ameongeza kwa kusema
“anaishukuru taasisi ya UN HABITAT kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI
kwa kutoa mafunzo kwa vijana wa VETA kuweza kuwapa mafunzo ya nishati ya
jua ili waweze kuindeleza katika miji inayokua pembezoni mwa mji wa Dodoma.”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment