RAIS TRUMP AWAKERA WAINGEREZA. - Mazengo360

Tuesday, 18 July 2017

RAIS TRUMP AWAKERA WAINGEREZA.

RAIS Donald Trump wa Marekani kupitia mpango wake wa kuzuia baadhi ya raia wanaotoka nchi za kiislam kutoingia Marekani kimewakera waingereza na kusema, akizuri Uingereza hatapatiwa mapokezi ya hadhi ya heshima  ya juu ilivyo desturi.

Trump+4
Rais Donald Trump wa Marekani.

Kulingana na gazeti la Uingereza la Daily Mail, Meya wa jiji la London Mhe Sadik Khan amesema Rais Dolnald Trump hatapatiwa mapokezi ya hadhi ya zulia nyekundi, kama  inavyofanyika kwa ma-Rais na viongozi wengine wa hadhi ya juu wakati wa ziara yake baadae mwezi huu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa Mayor.

Trump+3
Meya wa London Mhe Sadik Khan

Meya huyo wa London amekuwa katika vita vya maneno kwa muda mrefu na Rais huyo wa Marekani na hali imezidi kuwa tete zaidi baada ya tukio la kigaidi lililotokea mjini Manchester Uingereza mapema mwezi uliopita, na kisha polisi wengi kuongezwa mitaani kuimarisha ulinzi.
Baadae Rais Trump alitoa maoni yake kwamba hakukuwa na umuhimu wowote wa London kuweka polisi wengi kiasi kile mitaani, jambo lililowaudhi waingereza akiwamo Meya huyo wa London.
Kulingana na taarifa zilizoripotiwa pia hivi leo na gazeti la Daily Mail, limesema kwamba, Rais Trump amemtumia ujumbe Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa Mayor kumtaka acheleweshe kwa muda ziara ya mwaliko wake kwa Rais Trump nchini Uingereza alioutoa kwake mwezi Januari mwaka huu, hadi hali ikae sawa nchini mwake.

Trump+2
Watu yanao mpinga Rais Donald Trump nchini Uingereza.

Rais Trump amemtaka Bi Theresa Mayor pia awashauri makundi yanayo mpinga Rais Trump kuhusu ziara yake hiyo nchini Uingereza kutoa kauli ya kuondoa pingamizi hilo ili kuwezesha ziara hiyo, gazeti hilo limeripoti.
Mpango wa Rais Trump wa kuzuia raia toka baadhi ya nchi za Kiislam kuingia nchini Marekani unapingwa vikali na nchi pamoja na jumuiya za kimataifa ambapo Uingereza inaamini pia kwamba ni mpango wa kukandamiza demokrasia duniani.

Trump+1
Moja ya Raia wa Kiislam nchini Ungereza.

Uingereza ni moja ya nchi inayothamini haki za binadamu pamoja na kuheshimu demokrasia kwa ujumla, na pia ni nchini yenye idadi kubwa ya raia wa kigeni walioomba uraia wa Uingereza ambao pia wanatoka katika nchi za kiislam duniani.
(Taarifa na picha kwa hisani ya gazeti la Daily Mail la Uingereza).

MWISHO.