ZANZIBAR KUWA MWENYEJI KONGAMANO LA KISWAHILI. - Mazengo360

Breaking

Monday, 28 August 2017

ZANZIBAR KUWA MWENYEJI KONGAMANO LA KISWAHILI.

ZANZIBAR inategemewa kuwa mwenyeji wa kongamona la kwanza la kiswahili litakalojumisha nchi  wananchama wa jumuiya ya Afrika Mashariki baadae mwezi ujao.


Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Kiswahili Ukanda wa Afrika Mashariki Bw Kenneth Simala (mwenye tai) akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa wizara ya Habari mjini Kikwajuni, mkoa wa Magharibi  Zanzibar hivi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa wizara ya habari wa Kikwajuni mkoani Magharibi hivi leo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ukanda wa Afrika Mashariki Bw Kenneth Simala amesema Kongamano hilo litakuwa la siku mbili.
Amesema, “Kongamano hilo linalenga kukuza ushirikiano zaidi baina ya nchi wanachama ili kujiletea maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashari na linatarajiwa kuanza Septemba sita na kumalizika Septemba saba mwaka huu.
Katibu Mkuu huyo amefafanua zaidi pia kwamba nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki zina haja ya kukaa pamoja  na kushirikiana kupitia lugha ya Kiswahili ili kukuza zaidi  juhudi  za maendeleo katika  nchi husika na kukuza uchumi wa watu wa ukanda huu, alieleza zaidi.
Aidha, amevitaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika matumizi  mazuri ya lungha ya kiswahili na kuachana na maneno yanayokwenda kinyume na maadili na fasihi kwa ujumla ili kisaidie kuleta maendeleo zaidi.
Kongamano hilo linategemewa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa, waandishi wa habari, wasomi wa vyuo vikuu pamoja na  wajumbe kutoka nchi za Afrika ya Mashariki ambapo mada kuu ni mabadiliko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Kiswahili.

MWISHO.  

No comments:

Post a Comment