WAZUNGU NI WABAGUZI: ADAI MREMBO ALIYEJIBADILI JINSIA. - Mazengo360

Breaking

Friday, 1 September 2017

WAZUNGU NI WABAGUZI: ADAI MREMBO ALIYEJIBADILI JINSIA.

MREMBO Munroe Bergdorf WA Uingereza aliyejibadili jinsia toka ya kiume na kuwa ya kike mwenye asili ya Jamaika, amewashutumu wazungu kwa ubaguzi.


Mrembo Munroe Bergdorf wa Uingereza.

Bergdorf, 30, ambaye alikuwa akiwania tuzo ya mashindano ya urembo ya L’Oreal Paris huko UK amesema anajiona wa kipekee  katika mashindano hayo kwani ndiye wa kwanza kushiriki katika mashindano hayo baada ya kujibadilisha jinsia.

Mrembo huyo aliyekuwa akihojiwa na jarida la Vogue la Uingereza ameendelea kueleza kwa kulalamika kwamba alishangaa akiwa katikati ya maandalizi ya kampeni zake za kuwania taji hilo ndipo alipopokea email iliyomjulisha kwamba ameondolewa katika ushiriki wa mashindano hayo.



Aliendelea kusema kuwa baada ya kusoma taarifa hiyo alistaajabu na kuanza kulia na baadae kumfuta mama yake na kumjulisha hayo na kuanza kulia kifuani pake huku akijilaumu kuzaliwa mtu mweusi.
Mrembo huyo aliyekuwa akikimbiza katika mashindano hayo alibadili jinsia yake miaka minne ambapomuda wote kabla ya kujibadili alijulikana kwa jina la Lan. Amezaliwa na mamamwenye asili ya Uingereza na baba mwenye asili ya Jamaika.
Mrembo huyo alimalizia kwa kusema kwamba hakujua asili  au rangi ya mtu imeandikwa mgongoni mwake au katika damu yake au hata wakati wa kifo chake, hivyo amewashutumu wazungu kuwa wabaguzi wa hali ya juu kwa wengine.
(Taarifa zote na picha kwa mujibu wa gazeti la The Daily Mail la UK).

MWISHO.

No comments:

Post a Comment