SHARAPOVA AVUNJA UKIMYA. - Mazengo360

Breaking

Friday, 1 September 2017

SHARAPOVA AVUNJA UKIMYA.

MCHEZA tenesi toka Urussi Maria Sharapova amevunja ukimya tangu alipokutwa na kashfa ya kutumia dawa michezoni na kuwataka watu wamchukulie kama binadamu mwingine wa kawaida.

Mcheza Tenesi wa Urusi Maria Sharapova akieleza hisia zake

Sharapova, 30, alikutwa na dhahama ya kufungiwa kushiriki mashindano yeyote ya tenesi mwezi April mwaka huu ambapo alikuwa akitoa upinzani mkali kwenye mashindano hayo hususani alipokuwa akikutana na  mkongwe mwingine Serena William wa Marekani.

Mcheza Tenesi Maria Sharapova akiwa katika ubora wake.

Mchezaji huyo, alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu za aina ya “meldonium” kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo baada ya kushauriwa na daktari wake kutokana na kuwa na upungufu wa madini ya magnesium mwilini mwake, bila kujua zitamletea matatizo michezonu, alieleza Sharapova.

Maria Sharapova.

Sharapova anasema anajiona kuwa mfupi na mdogo mbele ya macho ya jamii japo yeye ni mrefu na kuongeza kwamba yeye na timu yake hawakuwa na taarifa endapo madawa hayo yamepigwa marufuku hadi vipimo vilipoonyesha.
Amewataka watu wamchukulie kama binadamu mwingine yeyote ambaye anaweza kukutwa na masahibu katika maisha hivyo wasimuone kama kituko, alimalizia mchezaji huyo.


(Picha na maelezo kwa hisani ya gazeti la The Daily Mail la Uingereza).

MWISHO.

No comments:

Post a Comment