MAKAMU wa Rais wa Zanzibar
Mhe Balozi Seif Ali Idd anategemewa kuwa mgeni rasmi siku ya kuwaenzi wazee
duniani itakayofanyika kitaifa huko Chwaka mkoani Unguja Zanzibar mnamo October
mosi, mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mhe Balozi Seif Ali Idd. |
Shamrashara za sherehe hizo tayari zimeanza na leo jumla ya wazee wapatao 70 wamepima afya zao kwa magonjwa yasiyoambukiza ya kiwamo kisukari, shinikizo la damu pamoja na dalili za saratani katika maeneo ya Sebuleni, Welezo na wilaya ya Kusini katika kijiji cha Paje.
Akizungumza
leo katika muendelezo wa shamrashara hizo za maadhimisho hayo uliofanyika kwa matembezi
maalum na kupima afya kwa wazee, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wazee iliyopo
chini ya Wizara ya Uwezeshaji Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhaza Gharib
Juma amesema wazee wana mchango mkubwa kwa jamii, hivyo wanapaswa kuenziwa.
Siku
ya Wazee Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo October mosi, na kwa Unguja kipindi
hiki itafanyika Chwaka na kauli mbiu yake ni “tusonge mbele kwa kutumia vipaji,
uzoefu, busara na ujuzi wa wazee kwa kuleta maendeleo ya jamii.”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment