MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa serikali
inaendelea kuhakikisha Mahakama hazijihusishi na vitendo vya rushwa ili kutoa
haki kwa mujibu wa Sheria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan. |
Mh. Samia ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha majaji na mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
‘Ninaamini,
nia ya kujenga mahakama bora na yenye kuaminika kwa Tanzania haiwezi
kutenganishwa na juhudi za serikali katika kuondoa umaskini na rushwa”
amesisitiza Mh.Samia.
Aidha
Makamu wa rais amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa kwa nchi kuwa na mahakama huru,
makini na yenye kuwajibika ipasavyo kwani mahakama huru ni msingi mzuri wa
demokrasia.
Alisema
kuwa pamoja na changamoto mbalimbali za mahakama uhuru wa mahakama ambao
ni umakini,uwajibikaji na utoaji haki kwa kufuata utawala wa sheria kwa
wananchi wake uko palepale.
Kwa
upande wa Tanzania Mhe. Samia amesema kuwa katika awamu ya tatu ya mapambano
dhidi ya rushwa ambapo kwa awamu mbili zilizopita serikali imefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kupunguza malalamiko yaliyotokana na ukiukwaji wa haki.
Katika
awamu ya tatu ya mkakati wa kupambana na rushwa utakaochukua miaka mitano
kuanzia 2017 hadi 2022, Tanzania itachukua uzoefu kutoka kwenye mkuatno huu wa
kimataifa kutoka kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola.
Kwa
upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Professa Ibrahim Juma alisema mahakama hiyo
iko huru na inatekeleza majukumu yake pasipo kuingiliwa na mtu yeyote na
akaahidi kuendelea kubadilishana uzoefu na mahakama za nchi wanachama ili
kuboresha utendaji kazi.
Aidha
Profesa Juma amesema Mahakama ya Tanzania kupitia majaji imekubaliana kuwa kila
Jaji atatakiwa kuhukumu zaidi ya kesi 220 ambazo ni asilimia 38 ya kesi
zilizoahirishwa mwaka 2012 hadi asilimia 5 Desemba 2016 na hii itafanyika kila
mwaka ili kujipima wao wenyewe kama moja ya malengo waliyojiwekea.
Akizungumzia mipango ya mahakama hiyo Profesa Juma amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2020 mahakama hiyo itakuwa imekamilisha ujenzi wa mahakama Kuu 13,mahakama za hakimu mkazi 14,mahakama za Wilaya 48,pamoja na mahakama za Mwanzo 100.
Mkutano
wa mwaka huu wa chama cha majaji na mahakimu wa nchi za jumuiya ya madola
umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini tangu Tanzania ijiunge na chama hicho
mwaka 1970.
MWISHO
No comments:
Post a Comment