RAIS na
Amri Jeshi Mkuu wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo ametangaza kutoa
kibali cha kuajiri vijana 3,000 katika JWTZ na akatoa angalizo lazima wawe ni
kutokea JKT.
RAIS na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. |
Pia Rais ametunuku
kamisheni mbalimbali kwa maofisa wapatao 422 wa JWTZ ambapo kati ya hao 31 ni
wanawake na 390 ni wanaume.
Rais aliyasema hayo leo akiwa
jijini Arusha ambapo kulifanyika maadhimisho ya kuwatunuku kamisheni maafisa
hao wa jeshi la JWTZ na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini.
Kulingana na taarifa fupi
iliyopatikana muda huu, Rais ametunuku jumla ya shahada na Stashahada za umahiri
jeshini kwa maofisa 11, Shahada 276 na Stashahada ya Juu kwa maofisa wengine
21.
Pia Rais ametunuku wahitimu
watano Shahada za kawaida na wengine katika ngazi ya masomo ya elimu ya kidato
cha 6, jumla yao wakiwa 109.
Aidha, ni mara ya tano kwa
Rais Dkt Magufuli kutunuku kamisheni kwa maofisa wa JWTZ tangu aingie
madarakani November 05, 2015, ila ni mara ya kwanza kufanya maadhimisho hayo
nje ya viwanja vya jeshi mfano vya Chuo cha Kijesha cha Monduli Arusha.
Hata hivyo, Rais Dkt
Magufuli inavyoonekana amevutiwa mno na utendaji kazi mahiri wa majeshi yetu ya
JWTZ na JKT kwani kazi nyingi muhimu na za dharura kwa sasa serekali imeanza kuwatumia.
Hivi majuzi juma hili wakati
Rais alipokuwa akizindua barabara yenye urefu wa kilomita 26 kutoka Uwanja wa
Ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Arusha kunakochimbwa
madini ya Tanzanite, Rais aliwaagiza SUMA JKT kufanya utafiti wa kujenga ukuta kuzunguka
eneo lote kunakochimbwa madini hayo ili kuzibiti wizi.
Rais Dkt Magufuli
anatarajiwa pia kulihutubia taifa katika maadhimisho hayo kutokea jijini Arusha
hivi leo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment