BAADA ya Msanii wa muziki
wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kukiri kuzaa mtoto
na mwanamitindo Hamisa Mobeto, hatimaye mama watoto wake Zari Hassan ‘Zari’
azidi kumuweka njia panda msanii huyo juu ya uhusiano wao.
Zari na Diamond wakiwa wamezama katika penzi mubashara. |
Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kupokea ushauri uliotolewa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.
“Watu
wakiamua kuchepuka au kudanganya ni sawa na kujipotezea muda, ingawa
wanahisi wanakuchezea wewe, hivyo usikate tamaa na usijilaumu kwa ajili ya
makosa ya wengine, maisha lazima yaendelee,”
“Mambo
yaliyotokea hayawezi kunipunguzia hadhi yangu, usijilaumu kwa yaliyotokea,
zingatia malengo yako na kufanya maisha yaendelee,” amesema.
Amesema
kuwa yale yote yaliyosemwa katika sakata hili yanabaki yalivyo na muda huu
anaamua kuyaweka kando na kuelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya sherehe ya
kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Sakata
hili limeibuka siku moja baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat
akionya asihusishwe na kitendo alichokifanya Diamond cha kuzaa na Mobeto.
Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond
amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto
aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo
tena.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment