SEREKALI
imesema
itaanza kutatua changamoto zote za utoaji elimu nchini kulingana na matokeo ya
tafiti husika na itawajumuisha wadau wote katika utekelezaji wake ikiwamo
kuziweka tafiti hizo katika tovoti za wizara zote mbili za Elimu na Tamisemi
ili ziwe wazi zaidi.
Kulingana na taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jana kwenye ufungaji wa mkutano wa siku nne wa kujadili maendeleo ya sekta ya elimu nchini kuanzia utoaji elimu ya awali, msingi, sekondar, vyuo vya ufundi hadi chuo kikuu serekali ilipokea mapendekezo mbalimbali na kuyajadili.
Akitoa taarifa ya
majumuisho ya maazio ya mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulika zaidi na Elimu, Tixon
Nzunda alisema mkutano huo wa mwaka huu ulikuwa wa mafanikio zaidi kiutendaji.
Moja ya yuliyojadiliwa na
kupitishwa ni pamoja na kupitia na kuidhinisha mpango wa maendeleo wa sekta ya
Elimu wa miaka mitano, (ESDP - 2016/17 hadi 2020/21) ambapo umeanza kutekelezwa
rasmi, Naibu Katibu Mkuu huyoamesema utalenga zaidi kutumia matokeo ya tafiti
nautakuwa wazi kwa wadau wote waumma.
Akifunga mkutano huo rasmi
jana katika ukumbi wa Hazina Dodoma, Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Musa
Iyombe aliwapongeza washiriki wa mkutano huo kwa kujadili kwa kina changamoto za
utoaji elimu hapa nchini na kuwataka wadau wote kuhakikisha yanafanyiwa kazi na
kutekelezwa kwani yataleta mabadiliko chanya katika sekta hiyo.
Kulingana na mapendekezo
yaliyowasilishwa kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo na
Mtandao wa Elimu nchini (Tanzania Education Network) walisema, wakati umefika
kwa serekali kupitia wizara ya elimu kupitia na kurekebisha sera ya sasa ya
elimu nchini ili iendane na wakati wa sasa wa utoaji elimu bure na kwa wote.
Mtandao huo wa mambo ya
elimu nchini walibainisha kupishana kwa kwa sera iliyopo ambapo haiendani
nakiwango cha rasilimali zilizopo ili kukidhi azma ya serekali ya utoaji elimu
bure na kuishauri serekali kupitia mkutano huo kuangalia upya uwiano wake.
Katika taarifa ya mapendekezo
hayo uliowasilishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano na mwenyekiti wa Bodi ya
Mtandao huo, John Kallage ilieleza baadhi ya mapungufu ya kisera ya sasa ambapo
mpango wa utoaji elimu bure umesababisha ongezeko la wanafunzi katika mashule
ingali rasilimali zilizopo ikiwamo waalimu,vyumba vya madarasa na hata huduma
zmuhimumfano vyoo kubakia kama zamani.
Maelezo ya mtandao huo
ulibainisha uwiano wa mwalimu mmoja kuhudimia idadi ya wanafunzi umebadilika na
kuleta changamoto kubwa ambapo mwalimu mmoja kwa sasa uwiano ni 1:164 kwa utafiti
wa mwaka 2016, na mwaka 2015 ulikuwa 1:99 kabla ya sera ya elimu bure kwa wote.
Sera ya elimu inasema uwiano ni 1:77, lipo ongezeko la uwiano takribani zaidi
ya mara mbili ya kiwango cha sera.
Changamoto nyingine iliyobainishwa
ni pamoja na kuhusu ufaulu wa wanafunzi kulingana na jinsia ambapo wanafunzi wa
kike tafiti zinaonyesha ufaulu wao ni mdogo kulingana na ule wa wanafunzi wa
kiume.
Akitoa takwimu hizo mbele
yamkutano wa ufunguzi Bw Kallage alibainisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi
wa kike nchini ni asilimia katika ya 5 hadi 6, ingali kwa wanafunzi wa kiume ni
asilimia 12 hadi 13 takribani mara mbili zaidi, hivyo kuwakandamiza wasichana
kutoka na jinsia yao.
Kallage alitaja sababu
zinazochangia ufaulu mdogo kwa wanafunzi wa kike ni pamoja na kutohudhuria masomo
shuleni au darasani kwa siku kati ya 40 hadi 45 kwa mwaka kutokana na kuwa
katika kipindi cha wanawake kuwa katika hedhi.
Wizara ya Elimu pamoja na
wadau wote husika wameshauriwa kuangalia njia ya kutatua tatizo hili la ufaulu kwa
wanafunzi wa kike ambapo ni la kijinsia, ikiwamo kujenga na kutenga
maeneomaalum ya maluwato kwa wanafunzi wa kike pamoja nakuhakikisha huduma ya
maji safi na ya kutosha pamoja na taulo za kike zinakuwe mashuleni, ili kuondoa
utoro na kukuza ufaulu wao.
Nae mwakilishi wa wadau
wote wa maendeleo wanaoshirikiana na Tanzania katika maendeleo ya sekta ya
elimu wanaotoka nje ya nchi wamefurahishwa na hatua za dhati za msingi kabisa
katika kutatia changamoto za utoaji elimu nchini na kuipongeza sana sereakali.
Akitoa hotuba kwa niaba ya
wadau wote wan je ya nchi wanaoshirikiana na Tanzania, Bi Janeth Tanya kutoka
Uingereza alisema sasa wanaiona nia ya dhati ya serekali kukabili changamoto
zilizopo.
Bi Janeth ambaye aliongea
kwa kutumia lugha zote mbili za Kiswahili na kiingereza katika hotuba yake
alisema, “wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Tanzania, wamefarijika sana kwa
hatua ya serekali kuandaa mpango wa miaka mitano wa maendeleo ya sekta ya elimu
(ESDP)unaojumuisha wadau wote na kufuata majibu ya tafiti na kuupongeza.
Bi Janeth alifafanua pia
zaidi kwamba suala la mimba za utotoni pamoja na baadhi ya jamii hapa nchini
kulazimisha ndoa za utotoni ni ni changamotoiliyokuwa ikirudisha maendeleo ya
jamii nyuma na kuongeza kusema kwamba lazima tabia hizo zipigwe vita kwa nguvu
zote ili kumkomboa mtoto wa kike.
Mkutano huo uliokuwa wa
siku nne uliazimia pamoja na mambo mengi kuweka wazi matokeo ya tafiti za
changamoto za elimu nchini, ambapo pia katika kuzikabili utajumuisha wadau wote
bila ubaguzi katika kuhakikisha huduma na miundo mbinu ya elimu inaboreshwa na
kuwa katikakiwango cha kutosha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment