JESHI la polisi mkoa wa Mjini Magharibi
limewakamata vijana wapatao 220 kwa kushukiwa kujihusisha na vitendo
mbalimbali vya kihalifu katika maeneo mbalimbali mkoa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharabi Hassan Nassir. |
Akizungumza leo na
waandhishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir
amesema vijana hao wamekamatwa katika wilaya tofauti za mkoa huo kufuatia agizo
la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud.
Mkuu huyo wa mkoa
alitoa agiza kwa vijana wapatao 336 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu
kujisalimisha wenyewe katika vituo vya polisi mkoani humo kupitia kwa masheha wa
maeneo yao.
Kamanda Nassir amefahamisha
pia kwamba vijana hao wamekamatwa kutokana na kuhusishwa na makosa mbalimbali
yakiwemo uvutaji bangi, ubakaji na uporaji mali za watu.
Kamanda huyo pia
amewasihi wananchi katika maeneo yote kutoa ushirikiano kwa polisi ili
kuwabaini vijana wote wanaojihusisha na ualifu ili kutokomeza wimbi la vitendo
hivyo nchini.
Hata hivyo, Kamanda
Nassir amefafanua kwamba jeshi la polisi litaendelea kuchukua juhudi mbalimbali
ili kuhakisha kuwa wananchi wanaishi katika hali ya amani na utulivu.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment