Wataalamu
wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa
kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka ambalo liliangushwa wakati wa
Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
![]() |
Wataalamu wa kutegua mabomu wa
Ujerumani wakiwa wameketi karibu na bomu hilo Jumapili.
|
Bomu hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi Jumatano.
Habari
hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa
wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.
![]() |
Watu waliohamishwa wanatarajiwa
kuruhusiwa kurejea makwao karibuni.
|
Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia nchini Ujerumani, na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa wa serikali.
Maeneo
ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend, na ni pamoja na
hospitali kadha, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki Kuu ya Ujerumani.
Inaaminika
kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita ambayo hayakulipuliwa
ambayo yametapakaa kote Ujerumani.
MWISHO.
(Taarifa na picha hizi ni kwa hisani ya BBC na AFP)
No comments:
Post a Comment